Bandeji Inayotumia Teknolojia ya 5G Yatengenezwa..Inauwezo wa Kutuma Taarifa za Maendeleo ya Kidonda Kwenye Simu..!!


Bandeji ambazo zinaweza kutambua jinsi kidonda kinavyopona na kutuma ujumbe kwa daktari itafanyiwa majaribio katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Bandeji hizo zitatumia teknolojia ya 5G kufuatilia na kutambua ni matibabu ya aina gani yanahitajika kwa mgonjwa.

Majaribio hayo yanafanywa na taasisi ya Sayansi ya chuo cha Swansea huko Wales nchini Uingereza.

Bandeji hii inatumia teknolojia inayofahamika kama nano, kutambua hali ya kidonda cha mgonjwa wakati wote.

Kisha itaunganisha kidonda na mfumo wa 5G kupitia kwa simu ya mkononi na kuonyesha vitu kadhaa kuhusu mgonjwa, kama eneo alipo na hali yake.

Wakati taarifa hiyo yote inakuja pamoja, teknolojia hiyo kisha itatambua aina ya matibabu mgonjwa ambayo anahitaji kuyapata.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad