Bongo Movies Walioandamana na Makonda Wazidi Kukosolewa...Cheki Bella Fasta Alivyowapa Makavu Live


Msanii wa muziki na filamu, Bella Fasta amefunguka kwa kud
ai kuwa hajapendezwa na kitendo cha baadhi ya wasanii wa filamu nchini kuandamana kupinga filamu za nje, kwa madai hatua hiyo ilitakiwa kujadiliwa na wasanii wote wa filamu na siyo vikundi vya watu fulani ndani ya tasnia hiyo.

Wasanii hao ambao waliandamana wakiongozwa na Jacob Stephan ‘JB’, waliiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kupiga marufuku wafanyabiashara wa filamu za nje kwa madai hawalipi kodi wakati wasanii wa ndani wanalipa 30% ya mapato ya filamu zao.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Bella amedai tukio hilo lilitakiwa kuwa na kauli moja ya wasanii wote wa filamu.

“Bongo Movie mmeniudhi, sana siyo wote, ni wachache,” alisema Bella Fasta kwa ukali na kuongeza “Yaani hamuoni aibu mnasema kabisa movie za nje zisiingie Tanzania, nchi gani mambo haya yapo?. Tufanye kazi nzuri ziuze siyo tunaingiza mambo ya siasa kwenye mambo yetu ya kawaida,”

Bella amesema, kama ilikuwa ni ajenda ya wasanii wote kuhusu kuibiwa kazi zao mbona wasanii wa muziki hawakuhusishwa.

“Kama hilo suala lingekuwa ni letu sote yanii wasanii wote tungeungana Bongo Movie wote au na wasanii wa muziki kwanini hawapo? au kuna kitu,” alisema Bella.

Steve Nyerere ni kati ya wasanii wa filamu ambao wamepinga harakati hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad