Ccm ,Cuf A na Cuf B Zilivyoichanganya Chadema Kwenye Ubunge wa Afrika Mashariki..!!!


Wakati wabunge saba kati ya tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala) wakipatikana juzi usiku, suala la wawakilishi wa upinzani limetawaliwa na hali ya kutoeleweka, huku ikibainika rasmi kuwapo kwa CUF  ‘A’ na CUF ‘B’.

Kikao cha juzi kilichotawaliwa na mjadala wa kikanuni kuhusu wawakilishi wa Chadema na CUF, kiliweka rekodi ya kuchukua muda mrefu baada ya kumalizika saa 7:00 usiku kikikipiku kikao kilichojadili sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow.

Waliopitishwa ni Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe na Alhaji Adam Kimbisa kutoka CCM, wakati Habib Mnyaa, aliyekuwa amevuliwa uanachama na CUF, alichaguliwa pia kuingia kwenye chombo hicho.

Hata hivyo, wanachama wawili walioteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Eala, Ezekiah Wenje, aliyepata kura 124 za ndiyo na 174 za hapana, na Lawrence Masha, aliyepata kura 124 za ndiyo na 198 za hapana, hawajaingia kwenye chombo hicho, kitu ambacho kimeifanya Chadema kwenda mahakamani.

Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema jana kuwa uchaguzi huo ulikuwa ni batili kutokana na taratibu kutofuatwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad