CCM Wamwaga Damu Kwenye Uchaguzi Mdogo wa Vijiji Kilombero/Ifakara..!!!


OCD Kilombero, Salaam!

Ninatoa pole kwa Askari Mwanamke,WP Huruma aliyepigwa kwa tofari kwenye paji la uso na kushonwa nyuzi tano siku ya jana, tarehe 23.4.2017, wakati akilinda na kudumisha amani katika kituo cha kutangazia Matokeo ya uchaguzi mdogo wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbasa Kati, mji wa Ifakara.

Tukio hili limetokea wakati bado tunakumbukumbu ya mauaji ya Askari wetu nane yaliyotokea huko Kibiti. Hali hii ya kushambulia na kuwazuru Askari wetu haiwezi KUVUMILIWA.

Ndugu OCD, ninatambua unamtambua aliyemjeruhi Askari wako kwani majeruhi amemtambua na wananchi mashuhuda wanamtambua. Anaitwa Max Temba. 

Ninatambua viongozi wake wa CCM wamekuja leo tarehe 24.04.2017 asubuhi ofisini kwako na kukulazimisha msimchukulie hatua za kisheria kijana wao aliyefanya tukio hilo.

Ninasubiri kuona maamuzi utakayochukua. 

P. Peter Lijualikali
Mb. Kilombero

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad