CHANJO ya Malaria Kutolewa 2018...!!!


Chanzo ya kwanza kabisa duniani dhidi ya ugonjwa wa Malaria inatarajiwa kutolewa katika nchi tatu za Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka 2018.

Chanjo hiyo ya RTS,S inafundisha mfumo wa kinga mwilini, kushambulia vimelea vya Malaria vinavyosambazwa na mbu, ambapo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, chanjo hiyo ina fursa kubwa ya kuokoa makumi kwa maelfu ya maisha.

Lakini haijafahamika kama chanjo hiyo itaweza kutumika kwa nchi ambazo zina huduma duni za afya. Chanjo hiyo inatakiwa kutolewa mara nne yaani mara moja kila baada ya miezi mitatu na dozi ya nne miezi 18 baadaye.

Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dk. Matshidiso Moeti, amesema chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa zaidi ya watoto 750,000 wenye umri wa kati ya miezi 5 hadi 17.

Licha ya mafanikio hayo makubwa, bado kuna visa vipya milioni 212 vya Malaria kila mwaka na vifo 429,000
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad