Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia
Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.
Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.
Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.
Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.
Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.
Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,
Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.
Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.