1. Kwanza mdomo wa mbu haupo kama sindano za kawaida zinazotumika, mlija wa mbu ambao hutumika kuingizia mate yenye vimelea vya malaria ni tofauti na ule unaotumika kufyonza damu kutoka kwa
binadamu, kutokana na hili kwaiyo damu tu ndio huingia kwenye mwili wa mbu kutoka kwa binadamu alieng`atwa na mbu, na mate tu ya mbu ndio huingizwa kwenye mwili wa binadamu.
2. Pili magonjwa yote ambayo huambukizwa na insekta kama, matende na malaria aya magonjwa yanaweza kusambazwa na mbu kwa sababu vimelea vya aya magonjwa huweza kujizalisha(multiply) katika mwili wa mbu, ambapo hivi vimelea huweza kusambaa hadi kwenye mate ya mbu baada ya hapo huweza kuingizwa kwa kung`atwa binadamu. Tofauti ni kwamba vimelea yani virusi vya ukimwi(vvu) vinapoingia kwenye mfumo mzima wa mmeng`enyo wa mbu humeng`enywa kama chakula cha kawaida kisha hutoka kama uchafu, ili virusi vya ukimwi viweze kujizalisha(multiply) ni lazima viingie kwenye seli maalumu za binadamu.
3. Tatu, virusi vinavyosabisha ukimwi huzunguka taratibu kwenye damu ukilingansha na vimelea vinavyosababisha magonjwa yatokanayo na insekta(mbu), hii inamaanisha ata mbu anaponyonya damu kwa binadamu ambaye tayari virusi vya ukimwi hawezi kunyonya idadi kubwa ya virusi. Tafiti zaidi zinaonyesha kwamba ili mbu aweze kueneza virusi vya ukimwi kwa binadamu mtu huyo ina bidi ang`atwe na mbu million kumi(10) idadi hii ya mbu ndio inaweza kutengeneza uniti moja(1) ya kirusi apo ndipo huenda kikasababisha kueneza vvu, hii inamaanisha ata ikatokea kwa bahati mbaya uka mmeza mbu aliye mng`ata binadamu ambaye ana virusi vinavyosabisha ukimwi huwezi kupata maambukizi.
UHIMU
Achana na ngono zembe kwani
huchangia kwa asilimia kubwa maambukizi
ya VVU ambavyo usababisha UKIMWI…