Harmorapa Hana Heshima Kabisa....Amchana Live Master J

Msanii wa 'hip hop' nchini Harmorapa amemchana mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo Master J kwa kusema hamtambui wala hadhani kama kama anaweza kuwa miongoni mwa 'Producer' walioweza ku-hit kwa ngoma kali Bongo.

Harmorapa anayetamba na wimbo wake wa 'Kiboko ya mabishoo' amefunguka hayo baada ya kutokea maneno makali ya mtayarishaji huyo kuwa Harmorapa hana kipaji cha muziki na kwamba si msanii bali analazimisha.
Kauli hiyo ya Master J ilionekana kuwachukiza baadhi ya wadau wa tasnia hiyo mpaka kupelekea meneja wake ambaye ni P. Funk kuingilia kati jambo hilo.
Harmorapa ambaye leo alikuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, ameulizwa kuwa anaichukuliaje kauli ya producer Master J, ambapo katika jibu lake, amesema kauli hiyo haimsumbui kwa kuwa anaamini kuwa ana kipaji, na kwa kuwa yupo kwenye mikono salama ya P Funk, anaamini atafanya makubwa kama walivyofanya wasanii wengine akiwemo Juma Nature.
Amekwenda mbali zaidi na kumpa makavu Master J kuwa si producer wala hamtambui kuwa miongoni mwa ma-producer wakali Bongo maana hakuna kazi yoyote aliyofanya ika-hit kama ilivyo kwa P Funk

"Kwa kaui ya Master J, sikujisikia vibaya kwa sababu najua kuwa mimi ni msanii, na rap kama wanavyorap wasanii wengine, yeye hamjui mtu kwamba baadaye anakuwa nani, ndiyo maana hata Majani ambaye yuko juu yake aliniona akajua mimi nina kitu akaniita akanielekeza.......Huyo Master J anaongea hivyo, hana ishu, hivi ni nani yule, mimi simjui, na sijui kama ni producer, naona hajui chochote na sijui kazi yoyote ambayo ime-hit kupitia mikono yake tofauti na ilivyo kwa P Funk..." Amesema Harmorapa
Akitaja wasanii anaowakubali zaidi Bongo, amesema kwa upande wa hip hop anamkubali zaidi Fid Q na upende wa kuimba anamkubali zaidi Alikiba. Kwa upande wa wasanii wa nje, amesema anamkubali za Lil Wayne, huku akimwagia sifa Diamond Platnumz kwa kuitangaza vyema Tanzania kimataifa

Akizungumzia mafanikio aliyonayo mpaka hivi sasa tangu ajulikane, amesema kubwa kuliko yote ni heshima anayopatiwa na watanzania hata wale ambao hawakuamini kama ni msanii kweli, pia fursa ya kuaminiwa na kushauriana na wasanii wakubwa Bongo kama Juma Nature, Prof Jay n.k.
Pia amesema mafanikio mengine ni fursa ya kufanya kolabo na msanii kutoka nchini Ubelgiji anayefahamika kwa jina la Critical, ambapo amesema Mbelgiji huyo alilazimika kumlipa pesa Harmorapa ili kufanya naye kolabo.
Kwa upande wa vitu, amesema mpaka sasa anamiliki nyumba na gari aina ya Morano yenye thamani ya shilingi milioni 35, ambavyo alipewa kama zawadi na bosi wake.
Ametumia nafasi hiyo pia kueleza jinsi ambavyo P Funk Majani amefanya kazi kubwa ya kubadili mtindo wake wa ku-rap, kutoka mtindo wa kizamani hadi ku-rap kisasa huku akimtia moyo na kuchukua jukumu la kumtengenezea ngoma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad