Hatarii..Ridhiwani Kikwete Atoa Povu kwa Serikali Juu ya Kukaa Kimya Sakata la Watu Kutekwa na Kupotezwa


Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameitaka Serikali kutokaa kimya na kutoa maelezo ya matukio yanayotokea nchini ili kuondoa wasiwasi na hali ya sintofahamu kwa wananchi.

Ridhiwani amesema hayo jana Bungeni, Mjini Dodoma wakati akichangia mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na bajeti ya ofisi ya Waziri mkuu kwa mwaka 2017/2017.

Ameitaka Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,  Mwigulu Nchemba kutokalia kimya matukio ya utekaji yanayoendelea nchini.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mie kwa maoni yangu siamini serikali wala upinzani. Rais kazungukwa na watu wanafiki waliomuweka pasipobudi baada ya Membe kutokupita. Na pia tunajua hao hao hawakupenda maneno yake wakati wa campaign.Je nitajuaje kama wao na hao wapinzani hawafanyi hizi njama zote wao wenyewe ili aonekane Rais kama gaidi. Tumeyaona haya yote kwenye nchi za west japo wanaziita conspiracy theory. Lakini ukifatilia undani yanaukweli. Na tangu Makonda kutaja majina ya watuhumiwa wa unga ndio kawa yumo kwenye kila laana ya uovu wa nchini. Niliyatuhumu haya kwa muda mrefu na nilipoona kushangiriwa kwa nguvu kule bungeni nikajua kuwa Rais Magufuli kazungukwa na nguvu kubwa inayotaka afeli asifanikiwe katika lengo lake la kuijenga Tanzania iwe nchi bora katika Africa. Na kama huu utekaji unafanywa na serikali basi Nnakuomba fatilia na uchunguze kwa makini sana kwani sio kila akuchekeaye anakutakia mema kuna wengine inawauma wakiona ukisifiwa kwa utendaji mzuri barani Africa. Usijeacha hii habari ya utekaji ije ikuharibie.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad