HAYA Maisha ya Mkenya wa Kawaida..Usidanganyike Ukaenda Kichwa kichwa..Utalia...!!!


Nimekaa Nairobi, Sehemu tofauti tofauti, nimejichanganya na wananchi wa Kawaida... Maisha yao ni magumu sana sana.....

Why?
1. Plot wanazoishi sio hygienic, choo kimoja hushea watu zaidi ya 30+ which is dangerous in case of disease epidimics

2. Nyumba ni za mabati, kama mabanda ya nguruwe, huwezi amini kumuona mtu mstaarabu kwa road but ukenda kwa plot yake ni ya bati kama nguruwe

3. Mitaa mingi haina maji, hutegemea maji yanayosambazwa na malori, Lori moja husambaza maji mtaa mzima, watu hugombania, ndio ya 20litre huuzwa 20bob=440/= Tsh... Wana wake hubeba maji mgongoni sio kichwani kama ngamia au punda wakitembea a distance.

4. Wachache sana wanao afford kula balanced diet, wengi hula mboga tu(sukuma, terere, kienyeji, etc kwa ugali, nyama ni adimu sana hula matajiri tu.....

5. Mb za Kenya huisha kama upepo na very expensive, Tsh 50/= (1110/= Tsh ) unapewa Mb-68 tu, ambazo ukilog in fb dk 10 zinaisha, wakati Tz Fb ni bure na Kwa Tsh 1500/= unapata 1GB and a lot of airtime for a week.

Hakuna vibando vya kupiga simu kama Tz, mfano Tz unaweza weka Salio ukanunua dk kadhaa za kupiga, Kenya Unaweka Salio na kupiga hivyo hivyo kavu kavu, kudadeki, Tz tuna unafuu mkubwa wa mawasiliano, huduma kama Halichachi Bando n.k zinasaidia wana nchi.

5. Uchafu na taka ni changamoto sana, wana nchi hutupa hivyo maana hakuna utaratibu maalumu kama magari, yapo machache but not affordable to wana nchi wa kawaida wa hali ya chini

6. NAULI kila city basi hujipangia haiko fixed na hakuna governing body yenye hupanga na kuamua nauli kama SUMTRA TZ... So naweza end a tao(town) kwa mbao(20bob=Tsh 440\=) lakini ujaridi kwa 70bob(=1500/= Tsh au soo(Tsh 2000/=) hii INA kufanya ushindwe kupredict

7. Wakenya hawasalimiani njiani, unapita kimya kimya unless uwe mnajuana ndo unaaema 'Sasa......" Tz ni waungwana ukipita kwa njia ni must utae hae juu waweza dondoka mbele akaja akakusevu uliyemuacha nyuma

8. Makelele MENGI sana, tao(town) juu magari yako MENGI sana hasa ya abiria, mahoni pipiiiii, it make the city look hooliganic... Tz uko poa juu mabasi yamepigwa stop kuingia city centre hata yakiingia yana location maalumu sio kuzagaa kama Nairobi

9. Matapeli yamejaaa, Ma conmen, ukiwa street kuibiwa simu ni kawaida, dk mbili unaoneshwa kisu, hasa Eastleigh kule, ni balaaa

1
Kwa Kifupi Maisha Ni magumu sana kwa RAIA wa daraja LA chini, but starehe kwa matajiri na wenye nacho

10. Mabangi yameharimu vijana, vijana waziwazi wanatafuna miraaa, na Rais Wao aliruhusu and promised to fund miraa projects, this is insane...

11. Makelele ya mziki ndani ya matatu yanaharibu sana maskio, na huwezi sikizana kwa phone ukiwa ndani ya matatu, regaae musics most preferred na matatu ziko equipped na music system nzito sound crazy for we non citizens who were not used to this before

Note:- This report is based in Society with low socioeconomic status which constitutes 75% of Kenyans in Nairobi

POSITIVE;- 
1. Shule zao ziko smart huwezi differentiate Gava na private
.2. Watoto wanatema ung'eng'e balaa, mtoto wa std 4 ni sawa na form 6 wa Tz,, they are very fluent, compentent in English both written and spoken......nashauri kwenye pesa wapeleke watoto Wao kula japo kwa primary, very cheap.....na quality uko juu

3. Magari ni rahisi kumiliki

4. Starehe nyingi sanaaaaaaa, sanaaaaa kama una pesa zako

5. Hakuna MTU anajali mambo yako, no kulogana au wivu...

6. Entertainments clubs, pubs zimejaaaa 

7. Mabasi yao yamepambwa sana this make the city jams look good 
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijapenda positive ya kupima ubora wa elimu kwa kujua kiingereza.

    ReplyDelete
  2. Sijapenda positive ya kupima ubora wa elimu kwa kujua kiingereza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad