Serikali nchini India yaizuia mitandao ya Twitter, Facebook na WhatsApp katika jimbo la Kashmir kwa muda wa mwezi 1 ili kurejesha hali ya usalama.
Hii ni kutokana na vurugu zilizozuka baada ya watu 8 kuuwawa na polisi ktk maandamano yaliyotokea wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Kashmir.
Kufuatia sekeseke hilo, inadaiwa wapinzani wa serikali walitumia fursa hiyo kusambaza kwa wingi picha kali zinazoonyesha wahanga na watu walioumizwa vibaya kwenye vurugu hizo, hivyo kuchochea vurugu zaidi.
Mitandao mingine iliyozuiliwa pia ni pamoja na Youtube, Skype, Snapchat, LinkedIn n.k.