Hii Ndio Sababu ya Wachezaji wa Yanga Kuachwa na Ndege Huku Uarabuni Baada ya Kichapo



Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ambao juzi walifungwa bao 4-0 katika mechi ya marudiano baina ya yanga na AC Alger kuwania nafasi ya kucheza makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Baada ya mchezo huo kuisha kwa Yanga kutolewa katika michuano hiyo, timu hiyo ilijikuta imekwama kurudi Tanzania baada ya wachezaji wake kuachwa na ndege nchini Algeria, Katibu Mkuu wa Yanga Mkwasa anasema kitendo hicho cha timu yake kuachwa na ndege ni kutokana na mawasiliano mabovu na wenyeji wao, pamoja na foleni.

"Sisi si mara ya kwanza kusafiri na usafiri huu pia kufuata ratiba tuwapo nje ya nchi . Tunauzoefu mkubwa tu na hili. Mawasiliano yetu na wenyeji wetu yamekuwa magumu kupelekea hali hii kutokea" - Alisema Boniface Mkwasa

Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga inasema kuwa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa walichelewa kwa uzembe wao si za kweli kwani wenyeji wao ndiyo walikuwa wazembe kwenye kukamilisha baadhi ya vitu muhimu.

"Kilichowafanya kuchelewa ni uzembe wa wenyeji wao kuwatafutia polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya road clearance.Taarifa hii ni tofauti na habari zinazoenezwa mitandaoni kwamba msafara huo chini ya katibu mkuu umefanya uzembe binafsi kuchelewa ratiba ya ndege . Wachezaji 12 pamoja na Katibu Mkuu ndio walioachwa na ndege ya Turkish Airline"

Wachezaji walioachwa na ndege ya shirika la Emirates ni kundi la kwanza . Utaratibu umekwishafanyika kwa kupatiwa usafiri kwenye ndege nyingine ya shirika hilo kwa ajili ya kuondoka kesho au keshokutwa kulingana na ratiba .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad