Hivi Ndivyo Ilivyokuwa Tukio la Kukamatwa Kwa Mwanamuziki Roma na Wenzake


Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Msanii Roma Mkatoliki akiwa studio na kupelekwa kusiko julikana, Muungwana Blog imefika katika studio za Tongwe Records jijini Dar es salaam ambapo mkasa mzima ulikuwa hivi...

Kwa mujibu wa Mashuhuda (Majina yanahifadhiwa) walio ambao pia wanaishi katika nyumba ambayo inapatikana studio ya Tongwe, wameijuza Muungwana kuwa April 5, 2017 ambayo ilikuwa ni jana, katika majira ya Saa moja jioni ilionekana gari aina ya Noah nyeusi nje ya studio hizo, ambapo walishuka watu zaidi ya Watano na kuingia ndani ya  studio hizo.


Watu hao bila ya kujitambulisha walitamka kuwa wanamuhitaji Roma na mwenzake ambapo walimchukua na kutoka nae nje, na baada ya muda kidogo walirejea ndani na kuwachukua wengine watano akiwemo na Prodyuza wa studio hiyo Anayeitwa Moni.


Mbali na kuwachukua watu hao pia mashuhuda hao wemeeleza baadhi ya vifaa vya studio hiyo pia vimebebwa ikiwemo TV, na Computer.


Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Studio hiyo  aliyejitambulisha kwa jina moja la Edin ameiambia Muungwana Blog kuwa nikweli tukio hilo limetokea na mpaka sasa hawajui Roma na wenzake wamepelekwa wapi na hivyo hawezi kuelezea zaidi mpaka atakapojua walipo wakina Roma, ambapo aliongeza kuwa anakwenda kuripoti katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini humo.

Hata hivyo saa chache baada ya tukio hilo kumekuwa na tetesi kuwa huenda kuvamiwa kwa studio hizo kumesababishwa na nyimbo  ya Tanzagiza ambayo imeachiwa hivi karibuni na Msanii Sifa Digital ambapo mwanzoni tu wa nyimbo hiyo linasikika jina la studio ya Tongwe Records huku maudhui ya nyimbo hiyo yaneikashifu serikali.


Hata hivyo uongozi wa Tongwe Records umekana kuwa kuhusika na utengezwaji wa nyimbo hiyo na kwamba msanii huyo ametumia "beat" ya Studio hizo bila wao kujua.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tongwe Records Junior Makame mnamo march 27, 2017 aliandika hivi kupitia ukurasa wake wa Instagram


"Sisi kama wanafamilia  na uongozi mzima wa TONGWE RECORDS tunasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kutumia midundo/ beats / instrumentals zetu za nyimbo zilizotoka kwa ajili ya kutengenezea nyimbo zao za kampeni wanazozijua wao wenyewe pasipo idhini yetu.. Tunaomba ambao washafanya hivyo wazuie kusambazwa kwa nyimbo zao hizo mara moja ili kutuepusha na lawama zitakazoletwa baada ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria kwa kukiuka haki zetu za kikatiba. 


Wenu ktk ujenzi wa taifa 

Junior ' J- Murder ' Makame. Oi"
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa ni vijana wakesho, CCM angalieni sana. Na uongozi wa Raisi msipuuze Vijana wala Watanzania. Huu ubabe wa kuchukua raia kama vinyago ulaaniwe. Wazungu wanatuibia Tanzania kupitia uomgozi mbovu. Vijana wanajaribu kujiajili na kutumia sanaa kuzungumza mnawaburuta kama vinyago. Je hii amri inatoka wapi. Wezi wa Escrow mliwaheshimu. Epa mliwaheshipu. Waliotorosha wanyama serengeti, mnawapigia magoti. Waliochukua mbuga za Watanzania kupitia Mazingira ni mabilionea mmewapa nchi na mali za Watanzania bure. Mtanzania anayehangaika kupata haki kila kukicha mbaroni. Tena mnawavamia usiku. Wapi Katiba yetu.Na nyinyi Wazee mnaoikalia Katiba uvunguni je hawa si Watoto au wajukuu zenu? au Watoto na Wajukuu zenu wapo CCM na wanakinga? Makonda yupo nje bado mkuu wa mkoa. Je Tanzania ni nchi ya wajinga au Wapumbavu? Lini wazee , maraisi, watafunguka au nao wamo.Ni aibu kubwa nchi yenye thamani na matumaini makubwa mnaenda kuwapigia magoti wawekezaji wa nje na kuwaburuta Watanzania wenye uchungu na nchi yao, mbona mnatuaibisha. Vijana hao muwajibu badala ya kuwakongota tena.Elimu ni mali< kosa kila kitu pata elimu ikusaidie maishani na kuiinua jamii yako kwanza. Mnawaomba Wazungu waje, hamuoni mnafukuzwa kwao? EHHHEEEEe. Inaumiza na kuaibisha vibaya sana. SIsi watu weusi tumekosa nini? mwimbaji sijui Remi aliimba, lakini wapi.Tunahitaji mzungu, Karne ya ishirini na moja. Ingawa babu zenu walipigwa, uuawa, peleka utumwani, bado unampigia magoti kumyanyasa mwanao. Natoa machungu yangu ya moyoni.Pole sana vijana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad