1. Utapata usingizi mzuri na mororo.
Kuvaa manguo mengi na kujifunika ma blanket kunaweza sababishia mwili wako joto hivyo uchelewe kupata usingizi mwili unahitaji mazingira cool ili upate kulala.
2. Unaupa mwili wako nafasi ya kupumua.
Kwa sababu muda wote wa mchana tunakua tumevaa nguo, inapofika muda wa usiku ni vyema tukauacha mwili upumue. Hasa kwa wanawake, kuvaa nguo za ndani muda wa kulala kuna sababisha vi bacteria na fungas kuwa traped. Watu wanaolala uchi wapo katika hatari ndogo ya kupata fangas sehemu za siri kuliko wale wanaolala wakiwa wamevaa nguo.
3. Kulala uchi pembeni ya mpenzi wako kunapunguza stress.
kwa wale wana ndoa, kulala uchi kunasababisha miili yenu igusane ngozi kwa ngozi kitu ambacho kinafanya miili yenu isiwe na stress. Pia hupunguza presha ya damu na kufanya muwe relaxed. Bila ya kusahau kulala uchi pembeni ya mtu unaempenda kunakufanya uwe mwenye furaha, hivyo kuwa na afya njema.
4. Utajisikia una ukaribu sana na mwenza wako.
Utafiti uliofanya huko Marekani unaonesha kuwa wanandoa wanaolala uchi huwa wanajisikia wapo karibu sana na wenza wao. Asilimia 57% ya wanandoa wanao lala uchi wame ripoti kuridhika na ndoa zao, huku asimilia 48% ya wanaolala na pajama wame ripoti kuridhishwa na ndoa zao. Kulala uchi kunakufanya ujisikie upo karibu na mwenza wako na pia bond nae zaidi.
5. Kulala uchi kunasaidia katika kupunguza unene (uzito).
Usingizi mbovu husababisha homoni za stress kuongezeka mwilini, na kuongezeka kwa homoni za stress katika mwili kunasababisha mtu uwe unakula vyakula ovyo hasa vile "junk food" ambavyo husababisha watu kuongezeka kilo na unene.
Tahadhari: Kabla hujaanza kulala uchi hakikisha mazingira uliyopo ni salama na yanakuruhusu wewe kufanya hivyo. Kwa mfano wale ambao wanaishi na roommates au ambao wapo hostel si vyema kulala uchi. Hakikisha upo mazingira salama ndio ulale uchi.