Hakuna ambacho kinaongeza joto katika mwili wa binadamu wakati wa baridi kama chai ya tangawizi.
Kutokana na kiwango chake cha juu cha Vitamin C, magnesiamu na madini mengine, tangawizi ni ya manufaa sana kwa afya ya bianadamu.
Tangawizi ni mmea ambao hutumika kama kiungo na pia hujulikana kwa sifa yake ya kutumika kama tiba.
Inaweza kutumika kama unga,kama mafuta, juisi au chai.
Tangawizi inafahamika sana kwa sifa yake ya ajabu ya kutibu magonjwa.
Tangawizi ni nzuri kutumiwa kama chai, tangawizi ni chanzo kizuri cha vitamini na madini kama vile vitamini C na magnesiam.
Kuna faida nyingi utakazozipata kwa kunywa chai ya tangawizi:
1. Huzuia Magonjwa ya Mtingishiko
Chai ya Tangawiziinawezakuzuiakutapika na kumaliza maumivu ya kichwa.
Pia inazuia kichefuchefu kinachotokana na mitingishiko ya safari za gari,meli au ndege.
Hivyo kunywa kikombe kimoja cha tangawizi kitaweza kusaidia kuepuka kichefuchefu na kutapika.
2. Inazuia Mchafuko wa Tumbo
Chai ya Tangawizi inasaidia mmengenyo wa chakula tumboni hivyo kuongeza kunyonywa kwa chakula tumboni na kuzuia maumivu ya tumbo yanayotokana na kula chakula kingi.
Pia huongeza hamu ya kula.
3. Hupunguza Uvimbe
Tangawizi chai inaweza kupunguza uvimbe wa viungo unaojulikana kama rheumatoid arthritis.
4. Hupambana na Magonjwa ya Kupumua.
Unashauriwa kunywa tangawizi kama unasumbuliwa na magonjwa ya kupumua kama vile mafua na kikohozi.
5. Huchochea Mzunguko wa Damu
Kunywa kikombe cha chai ya tangawizi kunaweza kukusaidia kuboresha mtiririko wa damu, kama vile kusaidia kuzuia mafua na homa.
6. Huongeza Kinga za Mwili
Chai ya Tangawizi ina chemikali za antioxidants zinazosaidia kuboresha mfumo wa kinga.
Kunywa kikombe cha chai ya tangawizi kila siku kunaweza pia kusaidia kuondokana na hatari ya kiharusi kwa kuzuia mafuta katika kuta za mishipa ya damu
Tangawizi pia imeonyesha mafanikio katika kupunguza viwango vya rehani (Chorestrol) na kuzuia kansa.
7. Hutuliza Msongo wa Mawazo
Tangawizi ina uwezo mkubwa wa kupunguza msongo wa mawazo kwa harufu yake nzuri ya kuvutia.
8. Inapunguza Matatizo ya Tumbo:
Inachochea kasi ya mmengenyo wa chakula kwa kuchangia kutolewa kwa asidi katika tumbo. Tangawizi inaweza kutumika kushughulikia tatizo la kukosa choo.
9. Husaidia Katika Kupunguza Maumivu:
Tangawizi chai inaweza kupunguza maumivu ya mwili na misuli.
Kunywa kikombe chachai ya tangawizi kila siku kunaweza kusaidia kuzuia maumivu yamisuli pia kusaidia kupunguza uchovu wa mwili.
10. Husaidia kwa Kuondoa Ugonjwa wa Asubuhi
Husaidia kupungua kichefuchefu kwa akinamama wajawazito kunakotokakna na ugonjwa wa asubuhi kwa kizungu “Morning Sickness”
11. Huboresha Nguvu za Uzazi kwa Wanaume
Tangawizi inasaidia kuboresha mbegu za kiume na nguvu za uzazi kwa wanaume kama ikitumiwa mara kwa mara. Pia inasaidia kutibu upungufu wa nguvu za kiume.
12. Kupunguza Uzito wa Mwili:
Tangawizi inasaidia sana katika kupunguza uzito wa mwili. Inasaidia kuunguza mafuta ya ziada katika mwili.
13. Kuongeza hamu ya Kula
Tangawizi inasaidia kuongeza hamu ya kula kwa kuchochea kutengenezwa kwa asidi za kumengenya chakula katika tumbo.
14. Husaidia kutoa Gesi.
Tangawizi inasaidia kutoa gesi chafu tumboni kwa njia ya asili.
15. Inasaidia Kupumua Vizuri.
Tangawizi inasaidia kufungua njia ya hewa na kukufanya upumue vizuri. Unaweza kuitumia baada ya kula kama kiburudisho pia.
Wanawake wajawazito na wale wenye tatizo la kutokwa na damu kirahisi wanashauriwa kupata ushauri wa Daktari kwanza kabla ya kutumia chai ya Tangawi