Huruma..Rais Magufuli Adondosha Chozi Baada ya Kusikia Msiba wa Mbunge wa Chadema,Atoa Kauli Hii


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli  amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndungai kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Dkt, Elly Marko Macha.

Mhe. Dkt Macha amefariki dunia jana Machi 31katika hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu

Vile vile Rais ameelezea kusikitishwa na kuhuzunishwa kifo cha Mbunge huyo ambaye ameondoka katika kipindi ambacho Taifa lilikuwa bado linahitaji mchango wake.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli amempa pole Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanachama wa CHADEMA kwa kuondokewa mwanachama wao na amesema anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemuomba Spika wa Bunge mhe. Job Ndungai kumfikishia salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huo.

“Mhe. Job Ndungai natambua kuwa kifo cha Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kimeleta mshtuko na huzuni kubwa siyo tu kwa Bunge bali pia kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, naomba kuwapa pole wote walioguswa na sote tumuombee marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina”. Alisema Rais Magufuli

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad