Ndo kwanza nimemaliza chuo maisha bado hajasettle kabisa, nahangaika tu na maisha Mara nimeajiriwa huku Mara kule. Huku nikiwa na extended family niliamua kuchukua gheto mitaa flani kwa sababu pia ya hali mbaya ya kuchumi nilichukua tu room moja nikanunua kwa Tv kangu nchi 14, jiko la mafuta na mkaa pia, nilinunua tu godoro dogo la nne kwa nne na kapet la plastic na mito miwili nikaanza kuishi gheto, hiyo nyumba ilikuwa na wapangaji 5 tuna share choo.
Nikiwa kazini dada mmoja sister du kweli akawa amenipenda sana na anataka tuwe karibu maskini nikawa nawaza huyu dada si ataniingiza hasara ambazo mi sikuwa nazihitaji maana mi nilishajizoelea gheto kwangu weekend napika mwenyewe isipokuwa siku nyingine za kati kati ya week.
Akawa analazimisha sana kuja kwangu nikamwambia kwangu sijui kama atapaweza naishi kigogo mazingira yangu nayajua mwenyewe, nikamchania tu ukweli kasema hajali ye anataka tu aje home apafahamu hata siku nikipata shida anifate.
Basi weekend moja nikamwambia njoo akaja dada wa watu.hata kumwelekeza ilikuwa shida maana nlimwambia akifika sehemu flani kuna uzwa mkaa kwa magunia akate kushoto mpaka kwenye kibanda wanachoonesha video baada ya hapo anyooshe mpaka kwa mama muuza mihogo mama Hadija apinde kushoto anyooke mpaka akikuta mtaro wa maji machafu hapo anisubiri nikamchukue yule dada alifanikiwa kweli nikaenda mchukua amechoka na jasho linamtoka make up imetoka maskini.
Nikatembea naye mpaka gheto kumkaribisha hivi namwona yupo fresh tu akajipumzisha chini kwenye godoro apulizwe feni zile za mezani angalau apoe kile chumba changu kina vidirisha vidogo vya kishkaji tu baada kama ya nusu saa salamu na utani akatoa kwenye begi lake khanga akavua suruali yake akaanza kwanza kuosha vyombo vilikuwa vichafu alipomaliza akawasha mkaa akauliza kama kuna mchele au unga vilikuwepo basi yule dada akapika pale na samaki kwa nazi mimi nimetulia tu naangalia tv kipindi cha marudio ya michezo.
Saa saba hivi kila kitu kikawa tayari tukakaa kwenye godoro tukapiga msosi. tukamaliza tukakaa kupiga story za hapa na pale mpaka mida ya saa 10 akasema akaoeshe vyombo akaenda akaosha akarudi tukawa tupo kwenye godoro namuuzia chai tu. Saa 12 akanambia anataka kuondoka nikamsindikiza akapanda daladala ilikuwa imejaa sana alisimama akaenda kwao masaki alifika kwao saa 2 usiku.
Jumatatu tukaonana kazini tukawa tunapiga story tukaenda lunch n.k next week akaomba tena aje kunitembelea sikuamini. Now ni kama miezi minne huyu dada bado huwa anataman aje kunitembelea pamoja na mazingira yangu kutokuwa conducive.
Nikawa nawaza huyu dada inawezekana vipi akawa interested nami? Na alikuja kipindi flani akaniletea rice cooker, tumeendaenda akaniletea badhi ya vyombo. Maskini nawaza huyu dada mbona angeweza kuwa na mwanaume ambaye ana pesa na vitu vingine vyote lakini kwa nini kaamua kwangu?
Tulishapima hana ugonjwa wowote, yaani hana tatizo na ni mzuri mpaka namwogopa. amekulia mazingira mazuri sana huko kwao kuna siku alinipeleka kwao ni kuzuri hasa ni zile family zinakula chakula cha draft yaani unachukua hapa, unachukua pale unachanganya na kule unapiga msosi ndani kwao ni baridi muda wote na sebule wanazo tatu katika nyumba moja sasa inakuaje anampenda msela kama mimi ambaye sijasettle kabisa?
HIVI WANAWAKE WA NAMNA HII BADO WAPO KWELI? Au anataka roho yangu? nashindwa hata kumwambia kuwa natamani ningemwoa maana daah ndo sasa naanza kujipanga kuhama huku uswahilini nihamie sehemu nyingine ya nyumba self at least vyumba viwili ananambia nibadilishe mazingira kidogo. NATAKA NIOE LAKINI NAWAZA KWA HUYU DADA HARUSI YA KITAJIRI MI NITAIWEZAJE?