Imefichuka...Hii Ndio Sababu Kubwa ya Mgomo wa Mabasi ya Kwenda Mikoni ..!!!


Chama cha Wamiliki wa Mabasi nchini (TABOA) kwa kushirikiana na Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima ili kushinikiza Serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kupitishwa siku ya Jumanne.

Mgomo huo utaanza leo Jumatatu.

Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa TABOA  ambapo Katibu Mkuu, Eneo Mrutu amesema sheria hiyo mpya inayotarajiwa kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki wa chombo cha usafirishaji na kupelekea mmiliki kufungwa jela.

Mrutu amewataka wabunge bila kujali itikadi zao kutopitisha sheria hiyo hadi itakapobadilishwa na kushirikisha wadau kwakuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad