JB Amchana Wema Sepetu na Wengine Ambao Hawakuandamana na Makonda Kariakoo


Muigizaji mkongwe nchini Jacob Stephen 'JB amefunguka na kudai hawakufanya maandamano ya kuzuia movie za nje ya nchi kuuzwa nchini bali waliandamana kuzitaka zilipiwe kodi au serikali itoe msamaha kwenye filamu za ndani.

JB amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na wanahabari wakati wa uzinduzi wa filamu ya Tunu na kudai kuwa watu wengi wamehusisha maandamano yao na siasa kitu ambacho hakina ukweli na kuongeza kuwa tasnia ya filamu kwa sasa inahitaji watu watakaowasaidia kumaliza kilio chao. "Sisi hatupingi movie za nje kuingia nchini, mimi mwenyewe nazipenda na ninaziangalia. Hapa ugomvi uliopo ni wao watozwe kodi au na sisi tuondolewe hizo kodi, wakifanya hivyo hakuna mtu ambaye atapiga kelele tena. Sasa hivi nakatwa asilimia 30 lakini bado natakiwa nitoe asilimia tano na wakati huo huo, nikitaka kutoa movie mpaka nikaombe kibali kama ni wewe ungekubali? Na jambo hili lisihusishwe na siasa kwani sisi mtu yoyote ambaye ataweza kutusaidia kutusemea tutamsikiliza hata akiwa wa upinzani hatuna shida" Alisema Jb

Aidha msanii huyo ameongeza kuwa wasanii wenzao wanaowakejeli kwa kuandamana wengi wao hawategemei movie kuwaingizia kipato na ndio maana wanaongea maneno ya ajabu huko nje. "Msanii yoyote ambaye filamu ndiyo chakula chake hawezi kuwa nje ya hili kwa sababu hataweza kuishi. Mimi niseme tu siwezi kuishi bila filamu ndiyo maana tunapiga kelele. Sitaki kuwataja majina lakini angalia tu wewe mwenyewe huyo mtu ambaye hataki kupiga kelele anaishi bila filamu?" JB alimaliza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad