Nyumba ni urembo, nyumba ni mapambo, ili nyumba iweze kuvutia inahitaji mazingira yenye hadhi ambayo yanaweza kumvutia mtu kwa muonekano wake wa nje na ndani pia inaweza kumvutia mtu kutokana na rangi za chumba.
Watu wengi huweka mazingira safi jikoni, sebuleni na kusahau kuwa chumba cha kulala pia kinatakiwa kuwa safi muda wote kwani ni sehemu ambayo inatumiwa kwa mapumziko.
Ili kuweze kupumzika vizuri baada ya mizunguko ya kutwa nzima ni vizuri chumba kikawa katika muonekano mzuri ambapo sambamba na hilo uwepo mpangilio mzuri wa nguo na fenicha.
Chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi, kinahitaki kuwa na hewa ya kutosha ili kumuwezesha mtumiaji kuweza kupata hewa safi pia inamsaidia mtumiaji kuweza kufanya usafi sehemu zote kutokana kuwepo kwa nafasi ya kutosha.
Epuka kujaza vitu vingi chumbani kama computer, meza viti, kapu la nguo chafu, kwani vitu hivyo vinaweza kuwekwa sehemu nyingine ya nyumba na chumba kubaki mahali pa kupumzika tu.