WABUNGE Waendelea Kuchezeana

Dodoma. Mazoea ya baadhi ya wabunge kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuzima hoja za wabunge wenzao, jana uliibuka tena baada ya Mbunge wa Makambako, Deo Sanga kuomba mwongozo uliozima hoja ya kutaja majina ya wabunge 11 wanaodaiwa kutaka kutekwa.

Sanga aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni 68 (7) pamoja na 64 A,B,C, alisema ndani ya Bunge yameongelewa mambo yanayohusu mahakama, usalama, mauaji na kutekwa.

“Nilikuwa nadhani kupitia kanuni hizi naomba mwongozo wako nini kazi ya  Bunge mheshimiwa naibu spika?” alihoji.

Mwongozo huo uliibuka baada ya Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Angelina Malembeka kuwataka wabunge waliosema kuna orodha ya wabunge 11 wanaotakiwa kutekwa kuwataja majina yao.

Hoja ya Malembeka ilimlenga Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ambaye siku za karibuni aliliambia Bunge kwamba ameambiwa na mmoja wa mawaziri kuwa kuna wabunge 11 watatekwa na Usalama wa Taifa.

 Hata hivyo, mwongozo wa spika ulioombwa na Sanga ulizima kiu ya Malembeka aliyetaka kumbana Bashe ataje majina ya wabunge hao 11, badala ya kutaja idadi pekee. Akijibu mwongozo wa Sanga, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliamua kupiga marufuku masuala ya Usalama wa Taifa kujadiliwa bungeni.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo hawa Wasiojiheshimu wakosa ya Maana kuanshisha Mijadala ya ubishano kama huu. Guys you are stealing our Valuable TIME, You need Time management awareness , Magu ,Tulia, Majaliwa ,Ndungai na Zungu "we needs to see changes with these Waheshimiwa who happened to be part of this priviledge to Call the as MP. Pia wapiga kura wanatakiwa kuelimishwa a Vote how worth it is to our comming GENERATIONs and the Country as a whole. Hapa Kazi TU

    ReplyDelete
  2. Hivyo hawa Wasiojiheshimu wakosa ya Maana kuanshisha Mijadala ya ubishano kama huu. Guys you are stealing our Valuable TIME, You need Time management awareness , Magu ,Tulia, Majaliwa ,Ndungai na Zungu "we needs to see changes with these Waheshimiwa who happened to be part of this priviledge to Call the as MP. Pia wapiga kura wanatakiwa kuelimishwa a Vote how worth it is to our comming GENERATIONs and the Country as a whole. Hapa Kazi TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad