Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro April 5, 2017 ameeleza sababu za Jeshi hilo kufananishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ katika utendaji wao wa kazi hasa katika ukusanyaji wa mapato.
Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi huo mbele ya Waandishi wa Habari akisema kumeibuka maneno sehemu mbalimbali hasa mitandaoni wananchi wakidai kuwa Jeshi hilo limeacha kazi yake ya kulinda raia na mali zao na kufanya kazi ya kukusanya mapato ambayo hufanywa na TRA.
“Nimeona watu wengine wanazungumza kwenye mitandao kwamba Polisi wamekuwa kama TRA. Mimi niliweke vizuri, sheria zipo. ukiangalia katika sheria ya Usalama barabarani iko vizuri. Na kama umekamatwa na kosa ambalo tunaamini umekiuka makosa ya Usalama barabarani hatukulazimishi wewe kulipa ile faini. Kuna mawili; kama hauko tayari kulipa ile faini, utaratibu upo tunakupeleka Mahakamani.” – Kamanda Sirro.