Hamis kigwangalla leo ameamua kufunguka kwa mwanaharakati Mange Kimambi huko Instagram baada ya mwanadada huyo kupost picha na maombi kibao kutoka kwa wananchi wakimwomba awasaidie kufikisha vilio vyao serikalini.
Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya mwanadada Mange kufululiza kupost picha na post mbali mbali zikionyesha hali mbaya ya huduma za afya kwenye baadhi ya hospitali zetu.
Nyingi ya post zinaonyesha jinsi wanawake kwenye baadhi ya hospitali kubwa ( including MUHIMBILI ) wakiwa wamelala chini sakafuni na watoto wao baada ya kutoka kujifungua, na baadhi ya post nyingine ni message anazotumiwa na watu mbalimbali wakilalamika jinsi wanavyopata tabu kupata huduma za afya mahospitalini .
Sioni sababu kwanini huyo muheshimiwa naibu waziri ya kumjibu huyo dada. Ni kupoteza muda wake na kujivunjia heshima yake. Vijana wengi wa kitanzania wakifika nchi za ng'ambo au ughaibuni kama wanavyoita sasa huwa wanajiona wanajua kila kitu hata maadili, heshima na busara na kibaya zaidi uzalendo hupotea kabisa. Au hata wale watanzania waliobahatika kupata watoto huku nje watoto wao wengi wamekuwa wakosefu wa adabu kuliko hata wamerekani wenyewe. Kwa maana hiyo kwa mfano kama tutaachiwa watanzania tuzaane na kuijaza marekani basi kipindi si kirefu marekani itakuwa ya hovyo kuliko Tanzania. Mtu mwenye kujitambua huwezi kukesha mitandaoni ukiwavunjia watu heshima zao kwa kisingizio cha uhuru wa kuongea.kuishi nje ya nchi isiwe sababu ya kupata kichaka cha kujificha kwa ajili ya kuwaporomeshea watu mitusi na kudharau kazi zao. Huwezi kuifananisha Tanzania na Marekani kwa takribani chochote utachokifahamu wewe kuhuduma. Marekani ina takribani miaka mia tatu ya kujitawala kutoka kwa muengereza. Ndani ya miaka mia tatu ya marekani ya kujitawala hakuna hata hatua moja inayopitia Tanzania ambao wao hawajapitia tena wamerekani katika kipindi cha miaka 50 tangu wapate uhuru wao hali ilikuwa zaidi kwa kifupi walikuwa hawana serikali ni vurugu tu.Yeye huyo dada kama kama kweli anauchungu na anayoyasema arudi tu nyumbani aonyeshe kwa vitendo iwe mfano wengine wamfuate sio kukalia umalkia wa mitusi mitandaoni kwani hajengi bali anabomoa na kujijengea maadui. Halafu anasubutu kusema na kukashifu kuwa Tanzania hakuna uhuru wa vyombo vya habari kama si upuuzi wake kitu gani? Huru wa habari isiwe sababu ya uvunjifu wa maadili ya watu. Kwa kifupi Tanzania watu wana uhuru sana wa kuongea wakati mwengine kupita hata Marekani. Kwa mfano huwezi kumuona mtu akithubutu kutowa maneno ya dharau kwa kifo cha askari kuuliwa atadakwa tu hata kama yupo nje ya Marekani. Na ukiangalia idadi ya raia wanaouliwa na polisi bila ya kosa lolote ni ya kutisha mno.
ReplyDeleteNaibu waziri una busara sana.
ReplyDeleteSERIOUS NAIBU WAZIRI UMEKOSEA SAANA HASA KUJIBU , KUNA MAMBO MENGI YA KUFANYA UTASIKIA MANGAPI UTAJIBU MANGAPI PLEASE FATA YALIYO KUPA DHAMANA DO THING RIGHT ON YOUR PART MATATIZO AYAISHI KAMWE KWA HILO UNAMWAIBISHA ALIYE KUTEUWA KWA KUJIBU MAMBO YA KWENYE MTANDAO
ReplyDelete