Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa Jumamosi April 8, 2017 atakuwa jimboni kwake ambapo atazungumza na wapiga kura wake kuwaeleza ukweli wa mambo yaote yaliyotokea.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nape Nnauye amendika kuwa, “Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17.”
Nape aliondolewa kwenye nafasi hiyo wiki chache zilizopita baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi ya Saa 24 aliyoiunda kufuatia Kituo cha Clouds TV kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Nape aliahidi kupeleka ripoti hiyo kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais John Pombe Magufuli ambapo siku iliyofuata Rais alitengua uteuzi wake na kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape.