Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo kinatarajiwa kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki kutokana na Bunge kukataa majina yaliyowasilishwa na chama hicho kwa ajili ya nafasi mbili za Chadema za wabunge wa Afrika Mashariki kwa madai kuwa chama hicho hakikuzingatia suala la jinsia.
Kwa mujibu wa Chadema kanuni zinataka theluthi moja ya wabunge wote (9) wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania na siyo kutoka kwa kila chama. Kesi ya msingi itataka tafsiri ya theluthi moja.
Maamuzi hayo yamefikiwa leo usiku na kikao cha wabunge wa Chadema waliokutana mjini Dodoma.