Mbunge wa Temeke Mh. Abdallah Mtolea amefunguka na kudai kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof . Ibrahim Lipumba ni msomi ambaye amejishushia heshima kwa kufanya jambo la ajabu la kuagiza vijana wake kuvamia mkutano wa CUF.
Mh. Mtolea amefunguka hayo alipohojiana na EATV na kudai kuwa Lipumba amefanya vitu vya ajabu ambavyo jamii iliyokuwa inamuheshimu sasa itampuudha na yeye atapunguza heshima aliyoitengeneza kwa muda mrefu.
"Mimi Lipumba ni kama kaka yangu kwa jinsi nilivyokuwa namuheshimu, lakini pia alikuwa kiongozi wangu bado namheshimu ila kwa kitendo kilichofanyika pale VINA nimeishusha heshima yangu kwake kwa kiasi kikubwa sana na niseme tu amekuwa mtu wa ajabu sana, elimu yake yotee na heshima aliyonayo amekuja kuiharibu kwa mambo ya ajabu kama yaliyofanyika"- Mh. Mtolea alifunguka.
Aidha katika hatua nyingine Mh. Mtolea amekiri kusikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi kuzuia mkutano wake uliopangwa kufanyika jana kujadili jinsi ya kuzitatua kero za wananchi na kuhusisha mkutano wake na masuala ya kisiasa kitu ambacho kinaweza kurudisha maendeleo nyuma.
" Ni kweli nilipanga kufanya mkutano na wadau wa maendeleo kujadili changamoto za wananchi wa Temeke haswa wale wanaoishi Kilakala ambao eneo lote limejaa maji, kwenye eneo lile tumelazimika kuweka pump inayonyonya maji lakini tulikuwa na changamoto kama mafuta na mambo mengine hivyo nilikuwa nimepanga kukutana na wadau mbalimbali kwenye ukumbi wa Temeke Executive lakini ghafla nashangaa nakuja kupewa taarifa nisifanye mkutano wowote kwa vile eti wamesikia nataka kukutana na vijana wa CUF ya Lipumba niwashawishi"- aliongeza Mh. Mtolea.
Mh. Mtolea ameendelea kusikitika kwa kudai kuwa kuzuia vikao kufanyika ni kuwanyima wananchi kutimiziwa haki zao za msingi.
"Mimi huwa ni mstaarabu nikitaka kufanya mkutano huwa nawajulisha jeshi la polisi na wao mara nyingi wamekuwa wakinipatia ulinzi tunashirikiana vizuri lakini hili la leo nilivyoenda kuwataarifu ni kama nimeenda kuwambia nizuieni. Hichi kitendo cha kutubana upinzani naona ndicho kinachoendelezwa zaidi, walitunyima mikutano ya hadhara wakaruhusu mikutano ya kujadili maendeleo na mimi siku zote huwa nafanya hivyo sasa nashangaa wamekuja na hii ya kuzuia vikao vya ndani bila kuuliza kikao kinahusu nini na wakati vinaruhusiwa. Hata kama ni kweli nilikuwa nakutana na watu wa CUF mimi ni Mbunge katiba ya chama inaniruhusu kufanya mkutano kwa sababu tayari kwenye chama nina uongozi"- alimaliza Mh. Mtolea.
ni awamu ya kishenzi hii
ReplyDelete