Kulala na Feni Kunaweza Kusababisha Kifo?

Watu wengi hasa wanaoishi katika maeneo yenye joto, mara nyingi hulala wakiwa wamewasha feni. Feni husaidia kupunguza kiwango cha joto katika chumba kwa kuongeza kasi ya mzunguko wa hewa katika chumba husika.

Wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kulala na feni, hasa katika mikoa yenye joto kama Dar es Salaam. Feni zimewafanya wafanyabiashara wa mikoa hiyo kunufaika kwani zimekuwa na wanunuzi wengi.

Kumekuwa na mijadala mbalimbali inayofanywa na wataalamu wa afya na hata watu wengine kuhusu madhara ya kulala na feni katika afya ya binadamu. Je ina hasara au faida gani kuitumia?

Wapo wengine waliodiriki kusema kuwa kulala na feni kunaweza kusababisha kifo cha ghafla kwa muhusika.

Feni kama vifaa vingine, itatumika ipasavyo basi inaweza kuwa na faida kwa binadamu lakini pia inaweza kuwa na madhara kwa baadhi ya watu.

Yafuatayo ni mdhara yanayoweza kumpata mtu anapolala akiwa ameiwasha feni.

Upungufu wa maji mwilini.

Hakuna hisia nzuri kama ile ya kupepewa na feni wakati wa usiku wenye jito kali. Usingizi huwa murua kwa vile hali ya joto imeshapunguzwa na feni. Na kama joto la chumba chako ni chini ya 35°C basi utafurahia uzuri wa hewa inayopulizwa na feni pasipo kukaukiwa na maji mwilini. Lakini joto la chumba chako linapozidi 35°C hewa inayopulizwa na feni huwa ni ya moto kuliko joto la ngozi yako na hivyo hukupelekea kutokwa na jasho jingi.

Kulala ukiwa unatokwa na jasho mara nyingi hupelekea kupungua kwa maji mwilini kwa kuwa wengi hatuna utamaduni wa kuamka usiku na kunywa maji ili kurudisha yale yaliyopotea.

Inaweza kuwaletea matatizo watu wenye Pumu (Asthma)

Hii hutokea kama huwa huna tabia ya kuisafisha feni yako. Ni kweli wengi wetu hatuna tabia ya kusafisha feni zetu. Lakini feni hukusanya vumbi lililopo chumbani na kulipulizia kwako, hii huwaathiri sana watu wenye pumu na aleji. Kama huamini angalia nyuma ya pangaboi za feni yako na utauona uchafu ulioko.

ili kuepuka kupuliziwa vumbi ni vyema ukawa na tabia ya kuisafisha feni yako mara kwa mara.

Maumivu ya shingo

Unapolala hali ya hewa ya chumba chako inakuwa ya joto. Hali ambayo inaweza kukufanya usilale vizuri. lakini feni inapokupuiza hupooza hewa na kukupa usingizi mzuri. Kwa kawaida hali ya hewa huanza kupoa majira ya alfajiri na feni inapokupuliza hupuliza hewa ya baridi kwako. Hewa hiyo ikiwa ya baridi sana huweza kupelekea misuli ya shingo kukaza na kukusababishia maumivu unapoamka.

Kulala na feni siyo kila mara huwa na madhara. Mara nyingine huwa na faida na hizi hapa ni baadhi ya faida za kulala na feni.

Kudhibiti kiwango cha joto

Inafahamika kuwa kulala katika chumba chenye hali ya hewa ya baridi hukufanya ulale usingizi murua na kwa muda mrefu zaidi. Feni inaweza kutoamsaada wa kuppoza hali ya joto ya chumba chako na kukifanya kiwe na mzunguko wa hewa safi hivyo kukupa usingizi murua.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watu engi hupenda kulala katika vyumba vyenye sauti murua kama vile sauti ya muziki laini, sauti ya mvua au hata sauti ya feni.

David N. Neubauer, profesa katika Chuo Kikuu cha Udaktari cha Johns Hopkins ameeleza kuwa anapenda kulala akiwa ameiwasha feni yake. “Hata kama hakuna joto, nitaiwasha feni yangu. Nikilala bila kuiwasha feni huwa napata wakati mgumu kuutafuta usingizi” alisema. Unapoiwasha feni yako izunguke katika mwendo mdogo, ile sauti yake husaidia kuondoa sauti nyingine zote zinazoweza kukusumbua wakati wa kulala.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad