Kwa hili la Halima Mdee kumtusi Spika, Tunakoelekea ni Kubaya zaidi

Nadhan hapa tunapasa kuweka itikadi zetu za vyama ,dini na kabila pembeni. kuna kipindi tunapaswa kusimama kama watanzania tukaweka mambo mengine yote mifukoni mwetu tukabaki na utanzania.

Tanzania ya sasa si tanzania ya jana...inabadilika inakuja na mambo leo ambayo mengine si mazuri. Nimemsikia mbunge mmoja akiongea lugha ya ajabu sana bungeni ambayo sitegemei mbunge msomi na ampambanaji ongee hata kama alikwazika sana. Angalau kistaarabu angeomba msamaha maana wanasema ada ya mja hunena uungwana ni vitendo.

Kwa mbunge kutamka maneno "fala" "mpumbavu" si maneno mazuri ingawa sishangai hili tatizo si kwa wabunge vijana tu . tulishawah sikia mtu mzima mmoja akiitwa wenzie "wapumbavu" si maneno ya kistaarabu tukiacha ashakum si matusi. Kuna lugha za mitaani hizo zisipelekwe bungeni kwa nini wabunge huwa hawapewe semina ya communication skills? maneno kama "kimenuka" "fala", "wapumbavu" hatutegemei kuyasikia bungeni.

Wapumbavu wote basi wanapotamkwa watamkwe pia na huo upumbavu walioufanya au nena wasiishiwe kuitwa wapumbavu. Nimesikitika sana kwa aina hii ya wabunge  ni wapi tulipokosea sisi watanzania?


Najua bado kuna watu watakuja kutukana hapa na kumtetea.Kudhihirisha kuwa tuna taifa ambalo either limeathirika na viroba au matumizi ya bangi lakini sisi wenye akili timamu hatutanyamaza.

 Tazama Video:

By Guru Master/JF
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaka kwani kusoma ni kuelimika? uenda hata angepata masters au Phd, haiwezi kumbadirisha silika yake hiyo ni kutokana na vinasaba kutoka katiak kizazi chake hadi hapo alipo. Kwa bahati mbaya sisi hatuna utaratibu wa kuwa na profile za watu mbali mbali sehemu za uzao wao, ndiyo maana wengine wanaonekana kama wantumia ulevi kumbe wapi ni kazi chao toka mababu walikuwa hivyo wana kasoro za kimaumbile na silika kama wendawazimu hivi. Sina hakika kama hii ni mara ya kwanza kufanya hivyo,na pia kulikuwa na tuhuma za masuala ya mapenzi ya jinsia moja, hebu tuwaangaliewanaume na wanawake wnaotuhumiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja tunwawasikia na kuwafahamu, uenda tukapata jibu, kufanya hivyo ni laana kwa muumba wetu na ndiyo baadhi yao wanaonekana kufanya mambo as if hawajitambui. Nimetoa hoja hiyo tuichangie tuache siasa za maji taka na uwayawani.

    ReplyDelete
  2. HAYO NDIO MADHARA YA BUNGE 'LIVE'.........JPM ALIONA MBALI, WABUNGE WANAISHI KWA 'MISIFA'....WATU WAZIMA HOVYOOOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad