Majina ya Nyimbo Yamfikisha Msanii Polisi..!!!


Msanii kutoka Arusha chini ya Weusi kampuni, Bonta Maarifa amedai kuwa mara nyingi majina ya nyimbo zake huwa yanampa matatizo kutokana na kuwa na utata

Bonta amebainisha kuwa jina la wimbo 'Nauza kura yangu' ilimfanya akapelekwa kituo cha polisi kipindi akiwa mwanafunzi wa chuo cha Mzumbe.

Leo akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio wakati akitambulisha ngoma yake mpya ‘Zero', Bonta amesema kuwa majina ya nyimbo zake huwa yanaendana na matukio yanayoendelea kwenye jamii kitu ambacho alipotoa ‘Nauza kura yangu' ilionekana kama anashawishi wanafunzi wenzake kuuza kura kinyume na maadili ya uchaguzi.

“Watu huwa hawanielewi sana wanaposikia majina ya ngoma zangu mpaka wasikilize nyimbo na kuzielewa, Nakumbuka hili swali ambalo naulizwa leo kuna tukio liliwahi kutokea miaka ya nyuma nilipotoa Nauza kura yangu, maaskari walikuja kunikamata wakanipeleka polisi kwa kosa la uhamasisha wanafunzi Mzumbe wauze kura zao kumbe sivyo nilivyomaanisha mpaka baadaye kuna baadhi ya viongozi walikuwa wanaelewa kitu nachokifanya ndipo wakaja kunitolea dhamana” Alisema Bonta.

Hata hivyo Bonta ameongeza kuwa wimbo wake mpya unaitwa 'Zero, kwa kuwa unahamasisha serikali iboreshe miundombinu ya elimu ili kupunguza idadi ya wanafunzi  wanaofeli mashuleni na siyo tu kung’ang’ania madawati wakati waalimu wanafundisha wakiwa hawana ari.

"Unajua wanafunzi wanaofanya vizuri wanakimbilia udaktari na kazi zingine za heshima anayepata daraja dhaifu ndiyo anaenda kuwa mwalimu, lakini wakati huo hata ualimu wenyewe umlipe vizuri hakuna kitu kama hicho kwa mfumo wa elimu wa hapa nyumbani tusitegemee Zero zikawa chache kuliko Division 1 hivyo mimi nimeikumbusha serikali ikazie macho suala la elimu na siyo vinginevyo" Bonta.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad