Chadema: Kasoro 10 Serikali ya Magufuli


KAMBI ya Rasmi ya Upinzani Bungeni imebainisha mambo zaidi ya 10 ambayo hairidhishwi nayo katika serikali ya awamu ya tano.

Kiongozi wa kambi hiyo,Freeman Mbowe, ndiye aliyataja mambo hayo wakati akiwasilisha hotuba yake bungeni juzi kuhusu makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Mbowe alisema mambo hayo ni pamoja na alichokiita uonevu wa viongozi na wabunge wa vyama vya upinzani akiwatolea mfano wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema).

Mbowe aliwataja wabunge Peter Lijualikali aliyehukumiwa kifungo cha miezi sita jela badala ya faini lakini hukumu hiyo ikatenguliwa na Mahakama Kuu na Godbless Lema.

Lema alinyimwa dhamana licha ya kuwa na haki ya kupatiwa na kulazimika kuwekwa mahabusu gerezani kwa takribani miezi minne.

Mbowe alizungumzia pia kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu na yeye mwenyewe kukamatwa mara kwa mara na Jeshi la Polisi wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisiasa.

Mbowe alitaja mambo mengine kuwa ni kupotea kwa baadhi ya watu katika mazingira ya kutatanisha na kutoa mfano wa msaidizi wake, Ben Saanane.

Aidha, Mbowe alisema, upinzani haufurahishwi na kutochunguzwa na kuchukuliwa hatua kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ana tuhuma za kutumia cheti cha kitaaluma cha mtu mwingine kujiunga na elimu ya juu.

Alisema mambo mengine wanayochukizwa nayo ni ukiukwaji wa demokrasia na utawala wa sheria kutokana serikali kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na kupiga marufuku urushwaji wa moja kwa moja wa vikao vya Bunge.

Aidha, Mbowe alisema, kitendo cha polisi kuua majambazi badala ya kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria ni kasoro nyingine.

Mbowe pia alidai kuna uonevu unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba wanaounga mkono vyama vya upinzani hususan Chama cha Wananchi (CUF), na kuwekwa kando kwa mchakato wa katiba mpya licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.

Mbowe pia alisema hali ya uchumi wa nchi ni mbaya huku akiishauri serikali kufanyia kazi onyo lililotolewa kwa Tanzania na Shirika la Fedha Duniani (IMF) hivi karibuni ili kuiepusha nchi kuingia kwenye anguko la uchumi.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, alitaka serikali ya awamu ya tano kutilia mkazo kilimo na mkakati wa kuinua uchumi vijijini na kusikitishwa na kupaa kwa Deni la Taifa.

Kambi rasmi ya upinzani pia haipendezwi na kasoro zilizopo katika mikataba ya kimataifa ikiwamo ya madini, changamoto ya ajira kwa vijana, kutozingatiwa kwa misingi ya sheria na haki za binadamu katika kushughulikia sakata la dawa za kulevya na utekelezaji wa kusuasua wa bajeti ya serikali kwa mwaka huu wa fedha.

FARU JOHN
Akichangia mjadala wa makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka ujao wa fedha juzi, Lema alisema ameshangaa kuona serikali inatumia fedha nyingi kupata ushahidi wa Faru John huku ikiacha kushughulikia kupotea kwa Saanane.

Mbunge huyo ambaye katika kuchangia kwake alilazimika kujibizana kwa kunukuu mistari ya kwenye Biblia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene, alisema anatamani kuona wabunge wakienda jela walau kwa miezi minne tu ili wakirejea kutoka huko, watakuwa wameachana na uoga na kutunga sheria zitakazonufaisha kizazi kilichopo na kijacho.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watanzania tuliokuwepo nje wengi tunajielewa sivyo kama huyo mpuuzi anavyoeleza. Kama ni uhuru wenyewe wa kuongea ni kutukana watu na kuwavunjia heshima zao kila kukicha utailaumu vipi serikali kuchukua hatua za kinidhamu? Kama serikali imeshindwa kumchukulia hatua za kisheria hayu malaya kwa kuwa yupo nje ya nchi kwanini wasivichukulie hatua vyombo vya habari hapo nchini vinavyosambaza mitusi yake? Au kwanini wasiblock account zake hata kuwataarifu Interpol kuhusiana na tabia mbovu ya huyo dada.udaku msitoe hii contribution yangu katika wachangiaji katika hii mada kama kawaida yenu lakini ujumbe utakuwa umekufikieni kwani mnaonekana kuyafurahia matusi yake huyu mpumbavu. Mdau NYC.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si wote wa nje wanakusapoti. Andika yyako mwenyewe si kwa niaba ya mtu. Kublock nini, unajua maana ya uhuru. Uko nje rejea jinsi watu wanavyokashifu serikali zao na maraisi wao. Uko nje wapi. Na kama nje bado unaishi kiuswahilini.Nawe haupo sophisticated, Umetoa matusi hadharani. Hakuna sheria Tanzania ya kumfunga mtu. Jifunze sheria zako pia uzijue kabla ya kuzungumza. Unaweza kaa nje usiwe mwerevu pia.Huyu dada ingawa haongei kiunadhifu anatoa point nyingi, kubwa na za maana. Jielimishe ujue Sheria za nchi yako vizuri. Kunasheria nyingi zinavunjwa Tanzania. Watu wanatekwa, Mkuu wa mkoa anavamia, Wakulima wanatapeliwa, We unawazazi na ndugu Tanzania au? huoni watu wananyanyaswa. Acha kujikomba. Umekaa nje kuna uhuru, huvamiwi na polisi usiku kwa kuikosoa serikali au Raisi. Usiwadanganye Watanzania wasiotoka nchini, wakati wanasoma magazeti online na wanajionea wenyewe. We ni CCM unayeandaliwa au kutaka cheo kwa upendeleo bila sifa? ndo maana Nchi inashuka kimaendeleo. Lini umeona Serikali za huko unakokaa kwenda Tanzania kuwatafuta Wawekezaji? Funguka.

      Delete
  2. kamkomesha hasaaaaa!! angeitaka amani kipindi anauza pete na cheni za mamake kwenda studio? kweli masikini akipata makalio hulia pwataaaaa!! ushasahau ulikotokea leo? kisa unaingia ikulu kama chooni, kwa mkuu wa mkoa kama WCB ofisi ndiyo uwaambie watu wakae kimya? wewe unakaa kimya kwa maslahi yako na upumbavu wako. unadhani ungefika hapo kama si hawa waTZ wanaonyanyasika sasa? mxxxx na wewe umekuwa kama waloenda kuchukua fomu peke yao, na kupiga kura walipiga peke yao na wake zao. mxxxxx tuondokee hapa katie mimba hewa huko!!!! ukalie kufananisha watoto midomo, kama wewe unajua kutangaza unayoyafanya ya misikiti na majengo ya masheikhe tuonyeshe na DNA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad