Maswali Magumu ya Kujiuliza Baada ya Mauaji ya Polisi, Kibiti - Pwani...!!!


Response ya Jeshi la polisi so far imekuwa ya kuonyesha hasira kuliko ya kimkakati. 

".... you don't shoot a cop, everybody wants a cop killer " .Haya ni baadhi ya maneno aliyoongea James Files, muuaji wa J. F. Kennedy baada ya kuulizwa juu ya muuaji wa afsa polisi J. Tippid. Mr. Files alimaanisha kuwa, hakuna mhalifu anayeua askari bila sababu za lazima sana kwasababu taasisi zote za kiupelelezi na kiuchunguzi zitamtafuta. 

Somalia na Sudan, silaha zinauzwa bei ndogo sana inasemekana. Tena hizi bunduki kubwa ndio chee kabisa kwasababu ya ugumu wa usafirishaji ukilinganisha na bastola. 

Sasa, katika mwangaza wa yote haya, ni nani na kwanini, atafute attention kubwa hivi na ugomvi karibu na taasisi zote za kiuchunguzi kwa mauaji ya polisi Kibiti ?
Hili ni moja kati ya maswali kedekede yanayoulizwa katika jukwaa hili na majukwaa mengine juu ya shambulio hili. 

Ili kupata majibu sahihi na kupiga hatua kwenye hili, ni muhimu kujiuliza maswali sahihi. 

MASWALI :
1. Kuna tukio lingine kama hili litakalokuja siku za usoni? 
Moja kati ya wajibu wa maafisa wa usalama ni kung'amua iwapo kuna uwezekano wa tukio jingine litakalo ambatana na hili. 
Kuna wakati kikundi cha kihalifu kinapanga tukio zaidi ya moja kwa kutumia wapiganaji wake waliosambaa maeneo mbalimbali. 

2. Je, tukio hili linahusisha mtu mmoja, watu wachache, au utekelezaji wake unafungamana na organization yeyote kubwa? 
Ni muhimu kujua kama washambuliaji ni sehemu ya network kubwa. Tukio lenyewe linaweza kuratibiwa na kutekelezwa na watu wachache, ila watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya kundi kubwa. 

3. Je, kuna uhusika wowote kutoka nje ya nchi? Vyombo mbalimbali vinaweza kuhusishwa kulingana na upana wa tukio. 
Ni muhimu pia kujua kama kuna taifa jingine linahusika katika tukio hili. Mara nyingi ushiriki wa taifa jingine unapuuzwa ila ukweli ni kuwa nchi jirani zinaweza kunufaika kwa namna moja au nyingine kwenye matukio kama haya.

4. Je, uhusika wa jamii kwenye tukio hili ukoje? jamii imechukia au imefurahi? 
Ni mara chache matukio kama haya yanaonyesha hisia za jamii, ila hii haina maana kuwa jamii haina uhusika. 

5. Je, maafisa wa serikali wamefanya makosa gani? Hii inaweza kukushangaza, ila serikali yako sio perfect. Ni kawaida kutafuta mchawi baada ya matukio kama haya japo, mara nyingi, udhifu katika kuzuia matukio kama haya huwa wa kitaasisi zaidi kuliko wa watu binafsi. 

6. Je, mabadiliko gani katika mamlaka ni muhimu baada ya mtukio kama haya? 
Sio kila wakati serikali inapokosea mabadiliko ni lazima. 
Kila mabadiliko yanakuja na gharama mpya na uwezekano mpya wa makosa. 

Pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. 
Pole kwa jeshi la polisi. 
Tunaweza kulishinda hili ndani ya misingi ya sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad