Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri majini na nchi na kavu (SUMATRA) Gilliard Ngewe amesema huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo nchini zitaendelea kama kawaida hapo kesho baada ya wamiliki wa vyombo vya usafiri nchini kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Makubaliano hayo yalifikiwa mapema leo baada ya wamiliki wa mabasi (TABOA), wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UWADAR) pamoja na wamiliki wamalori(Tatoa) kuzungumza na Profesa Mbarawa na kukubaliana kubadili kanuni na kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili.
Walikubaliana kuzifanyia marekebisho kanuni hizo ndani ya siku 14 na zipelekwe kwa wadau, pia zitenganishe makosa ya madereva na makosa ya wamiliki.