MBUNGE Ali Kessy Acharuka Bungeni...Ashangaa Roma Mkatoliki Kumtukana Rais na Kuachiwa Huru

Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili waache tabia hiyo

Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa. 
"Mtu anaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mpaka mwisho harafu anaachiwa nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtu unamtukana Rais unaachiwa aende Rwanda kule au nchi za kiarabu watakunyonga. Unamtukana Rais wa nchi wewe umekuwa nani? Uhuru gani huu, Demokrasi gani hii? Unaimba wewe nyimbo na mtu wa studio anarekodi ama kweli huu si utawala wangeniachi mimi dakika mbili ili niwaoneshe hawa" alisema Mbunge Kessy 
Keissy anasema ni jambo ambalo haliwezekani mtu kumuimba Rais anamtukana na wewe kuendelea kushabikai huku akidai kuwa yeye ameusikiliza wimbo wa Roma na kusikitishwa na kile kilichoimbwa.
"Ukiusikia huo wimbo wa Roma Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu sana, haiwezekani mtu na akili yako unasikia wimbo kama ule harafu unashabikia mtu, haiwezekani kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu Rais wa nchi hatukanwi popote pale haiwezekani nendeni nchi zingine, nenda Rwanda hapo nenda Burundi nenda DRC Congo ukaangalie watakushugulikia, nyinyi mnacheka cheka hapa. Rais haiwezekani kumchezea namna hii huu ni utovu wa nidhamu" alisisitiza All Keissy 

TAZAMA VIDEO:
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wasanii wamezidi eti sijui NAY WA MITEGO,ROMA MKATOLIKI,KARO JAREMIAH NAWENGINE WATAKAO THUBUTU WAKIONE CHA MTEMA MKUNI..HAWAJUI WALIFANYALO..WANASHADADIA NEGATIVE TU HAO MENGI MAZURI HAWAYAONI..TIA DISPLINE..MAGU

    ReplyDelete
  2. sio kessy sio ww hapo juu nyote n ma*ko.

    ReplyDelete
  3. So ungeaachiwa wewe ungemnyonga uko matekani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad