MC Algiers itawasili leo usiku jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.
MC Algiers imesafiri na wachezaji 18 huku ikilazimika kuwaacha majeruhi mabeki Azzi na Boudebouda, ambao wanategemea kurejea katika mechi ya marudiano jijini Algiers.
Kocha Kamel Mouassa ambaye hajashinda katika mechi zake mbili za kwanza alizocheza ugenini dhidi ya Bechem United na FC Renaissance amesema wanataka kufanya mabadiliko suala hilo "Ni ukweli kwamba hatujashinda mechi mbili tulizocheza Ghana na DR Congo; Siwezi kulificha hilo kwa wakati huu kwenu sababu tumekuwa tukishinda mechi za nyumbani.
"Tunajua haitakuwa kazi nyepesi kushindi ugenini, lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha tunashinda nyumban. Kama tukishindwa kuwafunga kwao tunatakiwa kufunga japo bao moja ugenini litatusaidia katika mechi ya marudiano, "alisema Mouassa.
Naye nahodha Hachoud alisema: "Tuna mechi mbili za kutufikisha hatua ya makundi, tunatakiwa kupata matokeo mazuro Dar es Salaam ili kufuzu kwa hatua ya makundi. Hatupaswi kufanya makosa katika mechi hizo mbili, iwe Jumamosi au hapa Algiers. "
Kikosi cha MC Algiers: Chaouchi, Chaal, Hachoud, Karaoui, Bouhenna, Mebarakou, Demou, Kacem, Chita, Derrardja, Seguer, Aouedj, Bouguèche, Nekkache, Djemaouni , Zerdab, Gourmi.