Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa wastani wa 1.4 kutoka asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Februari hadi asilimia 6.4 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya sababu zilizochangia ongezeko hilo ni kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula ambapo vyakula vilivyopanda bei ni pamoja na mchele, sukari, unga wa mahindi, mtama, ndizi pamoja na mihogo mibichi.
Kufuatia ongezeko hilo, baadhi ya wakazi Jijini Dar es Salaam wametoa maoni yao na kutaja ukosefu wa kipato kuwa unaongeza ugumu wa maisha hasa kwa wafanyabiashara ambao wamelalamikia upungufu wa wateja sambamba na ushauri wa hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.