Miaka 5 Sasa Bado Tasnia Ya Filamu Inakulilia...!!!


Leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Staa wa Filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ambapo ametimiza miaka mitano tangu alipoaga dunia Aprili 7, 2012

Kanumba anakumbukwa zaidi kwa mchango wake katika Tasnia katika kukuza na kuitangaza Bongo Movie ndani na nje ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Alikuwa chachu ya mafanikio kwa waigizaji wadogo na kutoa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii kwa wasanii wakubwa hapa nchini ili kuweza kutoboa kimataifa na kuweka heshima kubwa hapa nchini

Miongoni mwa filamu zake ni pamoja na, KIJIJI CHA TAMBUA HAKI, MAGIC HOUSE, FAMILY TEARS, MORE THAN PAIN, SATURDAY MORNING, OPRAH, WHITE MARIA, UNFORTUNATE LOVE, YOUNG BILLIONAIRE, NDOA YANGU, THE TWINS, MOSES, FAKE SMILE, RED VALENTINE, OFFSIDE, DANGEROUS DESIRE, BIGDADY, UNCLE pamoja na DAR 2 LAGOS.

Tangu kufikwa kwa mauti yake ni wengi wamekuja huku wengine wakifananishwa naye lakini hakika Kanumba atabaki kuwa Kanumba na kamwe hakuna atayekuja kufanana naye katika kila kitu.
Mungu azidi kuilaza roho yake mahali pema peponi. Amina.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad