Mkandarasi Aamriwa Kurudia Ujenzi wa Barabara

MKANDARASI wa barabara ya Kilindoni-Utende wilayani Mafia mkoani Pwani, ametakiwa kurudia ujenzi wa barabara hiyo kwa gharama zake mwenyewe.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau (CCM) aliyetaka kujua mkandarasi wa barabara hiyo anachukuliwa hatua gani.

Alisema, baada ya kufanya uchunguzi matokeo yaliyonesha kuwa baadhi ya sehemu za barabara hiyo hazijajengwa katika ubora unaotakiwa.

Ngonyani alisema, kutokana na hali hiyo mkandarasi alielekezwa kurudia kwa gharama zake mwenyewe maeneo yote yaliyoonekana yana upunguf kulingana na matakwa ya mkataba.

Kazi hiyo ya kurudia maeneo ambayo yamejengwa chini ya kiwango utaanza mara baada ya kipindi cha mvua.

Alisema uangalizi wa karibu wa maeneo mengine unaendelea kufanywa na Tanroads ili kuhakikisha kuwa barabara hiyo inakabidhiwa serikali ikiwa na viwango vya ubora unaokubalika kimkataba.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 14 ilijengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Limited (Chico) na kukamilika Januari mosi, 2015 na kufuatiwa na kipindi cha uangalizi cha mwaka mmoja.

Wizara kupitia Tanroads ilikataa kuipokea barabara hiyo kutokana na kasoro zilizojitokeza wakati wa kipindi cha uangalizi na iliamua ifanywe uchunguzi na kubaini upungufu huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad