Mkapa Afunguka Haya Mazito Kuhusu Aliyekuwa Kiongozi wa Freemason Tanzania..Adai Alimsaidia Sana..!!!


RAIS mstaafu Benjamin Mkapa ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mchumi mkubwa Tanzania na mzalendo Tanzania Sir Jayanti Chandelier( 89) ‘Andy Chande’ aliyefariki Alhamisi asubuhi mjini Nairobi, Kenya.

Taarifa kwa vyombo vya habari ilisema Mkapa amepokea taarifa ya kifo cha Chande kwa masikitiko makubwa. “ Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Sir J K Chandelier. Alikuwa raia muaminifu kwa Tanzania aliyechangia uelewa na ujuzi wake wa biashara kwa uchumi wa nchi,” alisema.

Alisema Chande alitumia muda mwingi kufanya shughuli za kijamii ambapo mchango wake katika kuhudumia shule ya viziwi Buguruni utabakia kuwa alama ya kihistoria. Alisema waliofanya kazi naye katika bodi za kampuni mbalimbali za binafsi na umma watamkumbuka kwa uwezo wake wa kuchambua matatizo na kutoa mapendekezo ya kuyakabili.

“Nimemfahamu kwa miongo minne tangu nilipokuwa Mhariri wa Magazeti ya TANU na serikali, wakati wa urais wangu na baada ya kustaafu kwenye shughuli za umma. Wakati wote alishauri bila chuki, hofu wala upendeleo,” alisema.

Aliongeza kuwa Chande atabakia kuwa mzalendo, atakayekumbukwa na familia na marafiki na urithi wake utabakia kwenye historia ya nchi. Maziko ya Chande aliyefariki baada ya kuumwa tumbo kwa muda mfupi kutokana na maambukizi, yatafaika Jumanne asubuhi katika makaburi ya Hindu, Dar es Salaam.

Msemaji wa familia, Joseph Mapunda alisema heshima za mwisho zitatolewa nyumbani kwake Barabara ya Msasani Namba 366a kuanzia saa 2:30 asubuhi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad