Mwanamuziki wa Ubelgiji Atua Nchini Kufanya Kolabo na Harmorapa..!!!


Mwanamuziki Kriticos kutoka Ubelgiji amewasili nchini kwa ajili ya kutengeneza wimbo wa pamoja na mwanamuziki  Harmorapa.

Kriticos ambaye anaimba miondoko ya kufokafoka, (rap) amesema ameupenda uimbaji wa Harmorapa  na ndiyo sababu ya kuamua kufanya naye kazi.

Aliyazungumza hayo muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere leo mchana.

Kwa upande wake Harmorapa anayetamba na wimbo wa Kiboko ya Mabishoo alisema ujio huo ni heshima kubwa kwake.

Harmorapa amewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea ngoma hiyo itakayotengenezwa na mtayarishaji wa muziki, P-Funk Majani.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mchezo mchezo huyu jamaa atapaa tushangae

    ReplyDelete
  2. Unatisha hamolapa!!! Chibu itabidi afanyw nini sasa???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad