Noma Sanaaa..Gwajima Kufikishwa Mahakamani Leo..Sababu Hi Hapa...!!!


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (47) na wenzake watatu leo wataendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Joseph Maugo alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa kesi ilipangwa jana kwa ajili ya utetezi na wapo tayari. Wakili mwingine wa Serikali katika shauri hilo ni Shadrack Kimaro.

Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala na Faraja Mangula ambao wote walikuwapo mahakamani jana lakini Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayeisikiliza kesi hiyo hakuwapo.

Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi.

Katika kesi hiyo, Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali katika usalama.

Washtakiwa wenzake George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya Berretta na risasi 20 kinyume na sheria.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bongo bhana kwa kutafuta sababu. wanaowatishia watu hawapelekw mahakamani wasiowashia wanawapeleka dahaa tutafika kwel

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad