Noma Sana..Pamoja na Wakenya Kwenda Mahakamni..Madaktari 470 wa Kitanzania Wajitokeza Kuchangamkia Fursa ..!!!


Wakati Mahakama nchini Kenya imezuia kwa muda madaktari kutoka nje kwenda nchini humo kupiga kazi, zaidi 470 wameomba kazi hizo kupitia Wizara ya Afya hapa nchini.

Serikali ya Tanzania imesema mchakato wa kupokea maombi hayo pia utaendelea kwa kuwa haijapokea maelekezo yoyote nchini Kenya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo.

“Tunasubiri taarifa rasmi kutoka Serikali ya Kenya kwa kuwa wao ndiyo walioleta maombi kwetu. Kama kuna mabadiliko yoyote, naamini watatufahamisha rasmi,” amesema.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya madaktari 470 wametuma maombi kati ya nafasi 500 zilizotangazwa za kwenda kufanya kazi nchini humo.

Msemaji wa wizara hiyo, Nsanchiris Mwamaja amesema: “Tumepokea maombi mengi ya kutosha, lakini ikitokea mtu akatuma tunayapokea, hivi karibuni jopo litakaa na kuanza kupitia maombi hayo kabla ya usaili na baadaye kupanga mipango ya namna gani watafika vituo vyao vya kazi.”

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sasa hivi wewe kwa akili yako ndogo unadhani kiingereza ni lugha ya ajabu?.watu wanawezaje kuwa madoctor wasijuie english .tuondole uupuzii wako .watu wanauza maatunda na mchicha barabarani na wanaongea english language .durban south africa na hawajui kusoma wala kuandika ,sembuse hao madoctor.kwa hatukuwaomba msaada .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad