Ndugu zanguni kuna tabia ambayo imezoeleka miongoni mwa wengi kila waonapo nyoka wanawapiga na mawe,magongo na silaha aina yeyote ile mpaka wanawaua hata pale nyoka akiwa sehemu pekee yake ametulia bila bughudha yeyote ile ila utashangaa mtu anaanza kupiga yowe na kuita kadamnasi ya watu na kisha kumshambulia nyoka ambaye alikuwa amejituliza zake tu.
Kwanini tunawachukia kwa kiasi kikubwa nyoka?
Watu wanadai Nyoka ni adui ya binaadamu lakini tusisahau sisi ndio tunaojenga uadui nao sababu kila tukiwaona tunaanza kuwashambulia hata kama hawakuwa na kosa ya aina yeyote ile
Mfano hawa nyoka wa majumbani green snake au black snake ambao kipindi cha baridi hukimbilia majumbani kwa watu kutafuta joto.
Nakumbuka nilivyokuwa mdogo maeneo ya Mbeya hawa nyoka walikuwa na tabia ya kuingia ndani kutafuta joto na hawakuwa na nia yeyote ile mbaya lakini cha kushangaza huyo nyoka akionekana watu huanza kupiga yowe na kisha anauliwa kikatili badala ya kupewa msaada wa joto,anakimbia shida na anakutana na dhahma.
Ili kuthibitisha nyoka ni marafiki zetu na sio maadui wetu nadhani wengi ni mashahidi kuna wakati nyoka akikimbia baridi na kutafuta hifadhi yenye joto hukimbilia majumbani na wakati mwingine hujibanza karibu na mtu ,wangapi wanalala na nyoka bila ya kujijua?na wengine wakishafahamu wamelala na nyoka wakistuka wanaanza kupiga yowe kisha kumuua nyoka huyo.Inashangaza sana huyo nyoka angetaka kukudhuru basi angekudhuru kitambo sana kwani hajui kama amejibanza karibu na mtu?
Kwani harufu ya mtu haifahamu lakini kutokana hakubughudhiwa na yeye shida yake ni joto hivyo ameamua kujisogeza karibu na shuka apate joto akishapumzika anakwenda zake..lakini sie tunachowafanyia sio haki kabisa
Pia ni kesi ngapi tunashuhudia watoto wadogo wakicheza na nyoka tena muda mrefu bila kudhuriwa ,sababu haswa nyoka sio adui na mtoto hajui kudhuru
Kwa hizi sababu mbili tufahamu nyoka ni rafiki na sio adui lakini rafiki maisha yake yakiwa hatarini lazima ajilinde na njia sahihi ya kujilinda ni kushambulia
Nawasihi ndugu zangu sio kila tukimuona nyoka tunapiga mayowe na kuanza kutafuta mawe,fimbo na kuanza kuwashambulia ,sisi ndio tunawafanya wakasirike lakini nyoka ni marafiki haswa nyoka wa majumbani hawa na pale wakitafuta hifadhi ya joto tusiwadhuru
Mie hawa nyoka wamenisaidia sana kunisafishia shamba na nyumba ,wadudu kama mende ,panya na aina wafananao wameisha sababu ya hawa home snakes wana msaada sana.
Mwandishi utakua mchawi sio bure, kweli umuone nyoka ndani umchekelee tu, kawa mjombako?
ReplyDeleteHuyu atakuwa kizazi cha nyoka sio bure. Unatokwa povu jingi kutetea nyoka?? Maandiko matakatifu yameweka wazi mahusiano ya mwanadamu na nyoka. Usitake kutulisha ufahamu wako haba. Soma kwanza kisha ufundishe
ReplyDelete