Tume ya Maadili ya Utumishi wa Viongozi wa Umma yakubali mashtaka dhidi ya RC Makonda yaliyopelekwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo.
Moja ya mashtaka yaliyowasilishwa ni tuhuma ya RC wa Dar, Kugushi vyeti vya kitaaluma kulikofanywa na RC makonda huku akijua fika kuwa vyeti anavyotumia vya taaluma si vyake wala si muhusika hivyo kujiita PAUL CHRISTIAN MAKONDA huku akijua fika kuwa yeye ni DAUDI ALBERT BASHITE, amekiuka sheria za nji nakutenda jinai.
Pili ni Kula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Mheshimiwa Rais kwa kutumia jina la kugushi.
Tatu ni kujipatia mali kama magari na vinginevyo kinyume na maadili ya viongozi wa umma, ambapo zawadi zote unazopokea unapaswa kutangaza hadharani, ikiwemo kupata mali hizo kwa wahusika ambao amekuwa akiwatangaza hadharani na kuwatuhumu kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Nne ni kukiuka Misingi ya utawala bora haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kutuhumu watu ovyo hadharani kuwa walijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kabla ya kukutwa na hatia na kisha wengine kuachiwa huru baada ya kubainika hawakutenda makosa hayo; kinyume kabisa na sheria ambapo mtu anatakiwa kutangazwa hadharani anapokutwa ametenda makosa.
Na tano ni uvamizi wa kituo cha kirusha matangazo ya redio na runinga cha Clouds media, ambapo akijua kuwa maadili ya viongozi wa umma, hayaruhusu kiongozi kushurutisha au kulazimisha jambo lolote kwakutumia madaraka yake kama kiongozi, ambapo mtuhumiwa alitenda kosa la kutaka kutumia nguvu kurusha kipindi.