POLISI Wapiga ‘Stop’ Kikao cha Mbunge CUF na Maalim Seif Shariff..!!


JESHI la Polisi Dar es Salaam limezuia kikao cha Mbunge wa Temeke (CUF) Abdallah Mtolea, ambao ulipangwa kufanyika leo kutokana na sababu zisizofahamika.

Jana Mtolea alithibitisha kufanyika kwa kikao hicho ambapo mkutano huo ulitarajiwa kuhudhuliwa na Katibu Mkuu CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

Juzi Aprili 22 mwaka huu, watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahimu Lipumba, walivamia mkutano wa wafuasi wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na kuwapiga na kuwajeruhi wenzao pamoja na waandishi wa habari.

Lengo la Mkutano huo ni kufanya harambee za kuchangisha fedha kwa ajili ujenzi miundombinu ya ebneo la kilakala hasa wakati wa mvua.

Taarifa alizozipata kutoka polisi zilidai kuwa Mtulia alipanga kuwakusanya wafuasi wa lipumba na kuwashawishi kuhamia kwa maalimu kitu ambachom si cha kweli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad