Serikali ya Rais Joseph Magufuli imeiomba Kenya kuisaidia kumkamata Mr Bashir Awale, afisa wa zamani wa benki, nakuchukua maelezo.
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, George Masaju alimwandikia mwenzake wa Kenya Githu Muigai chini ya Msaada wa Sheria wa Pamoja (MLA), akimtaka ampatie mtu huyo ili atoe ushahidi miaka miwili baada ya kufukuzwa nchini.
Awale anatuhumiwa kwa kutoa fedha ili kuwashawishi maafisa wa serikali kuzipendelea benki mbili wakati Tanzania ilipotangaza dhamana ya kimataifa mwaka 2012.
“Tumepokea ombi la MLA na tunalifanyia kazi kwa ukaribu na ofisi Sheria ya Nchi sambamba na ombi. Timu ya wapelelezi kutoka Tanzania na Kenya imewekwa katika nafasi ya kutekeleza ombi,” Mkurugenzi Mtendaji wa EACC Halakhe Waqo alisema.
Hata hivyo mkurugenzi Mkuu wa EACC, hakutoa maelezo juu ya kalenda ya matukio ya kazi yao na kama ameshamwita mtuhumiwa.
“Itachukua muda. Kwa sasa, hatuwezi kuwapa maelezo yeyote lakini naweza kuwahakikishia itafanyika hivi karibuni.”
Bashir alikamatwa Desemba 2015 na kufukuzwa nchini juu ya madai ya kukaa kinyume cha sheria. Alisemekana kuwa ni miongoni mwa wanachama wa timu ya kampeni za Urais za aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alishindwa na Magafuli. Dar es Salam waliitaka Nairobi kumshikilia Bashir na kuchukua maelezo ya ushahidi wa madai ya kauli inayoonyesha kuhusika katika kashfa hiyo.
Watanzania watatu tayari wameshtakiwa kwa makosa saba ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha kwa njia zisizo za halali, kughushi, matumizi mabaya ya nafasi, rushwa, na kwa sasa wako mahabusu.