Raia wa Kigeni Nchini Wapewa Siku 90..!!!


Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imetoa siku 90 kwa wageni kufanya uhakiki wa vibali vya ukaazi ili kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi nchini pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala baada ya uzinduzi wa mfumo wa uhakiki kwa kutumia njia ya kielekroniki amesema mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa waajiri na wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na mamlaka husika.

Dkt. Makakala amezitaka taasisi na mashirika binafsi baada ya kuhakiki vibali vya wageni wao watatakiwa kuwasilisha taarifa za vibali hivyo katika ofisi za Idara ya Uhamiaji za mikoa zilizopo karibu na ofisi hizo ambapo amesema baada ya muda huo kuisha wale wote ambao hawajahakiki hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa nchi Gani njaa utekaji umasikini.pyeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad