Rasi..Msajili Akubali Maalim Seif Kufukuzwa Cuf..!!!


OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, imebariki ombi la Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi(CUF) Taifa Profesa Ibrahim Lipumba la kumkaimisha Ukatibu Mkuu Magdalena Sakaya.

Hivi karibuni Profesa Lipumba alitangaza kumvua madaraka hayo Maalim Seif Sharif Hamad, kwa madai kuwa amekaidi wito wake na kususia ofisi kwa miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa barua iliyosambaa  jana kwenye mitandao ya kijamii, imeeleza kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imejiridhia kisheria na kukubaliana na ombi hilo baada ya kupitia vifungo vya Katiba ya CUF.

Barua hiyo ambayo imeandikwa Machi 21, mwaka huu  yenye kumbukumbu namba HA.322/362/14/74 imetiwa saini na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza imemtaka Profesa Lipumba kurejea barua yake yenye kumbukumbu namba ya CUF /AK/DSM/MKT/02/2017 ya Machi 16,  mwaka  huu.

“ Msajili wa Vyama vya Siasa amepokea taarifa  uliyowasilishwa kuhusu Magdalena  Sakaya kukaimu  nafasi ya Katibu Mkuu wa CUF kwa mujibu wa ibara ya 93(3)ya Katiba ya CUF toleo la mwaka 2014, kutokana na Maalimu Seif  Sharif  Hamad kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“ Ofisi imesoma Katiba ya Chama chenu (CUF)  na kujiridhisha kuwa ni kweli kwamba ibara ya 93 (3) imeelekeza hivyo.     Hivyo , Ofisi ya Msajili  wa Vyama vya Siasa itampa ushirikiano unaostahili Magdalena  Sakaya  katika kutekeleza majukumu ya Katibu Mkuu wa CUF,” barua hiyo imefafanua.

Akithibitisha kupokewa kwa barua hiyo Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya, alisema barua hiyo wameipokea.

Kambaya ameshangazwa na kitendo cha watu kuipiga picha barua hiyo na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii wakati jambo hilo linahusu mambo ya ndani ya chama.

“Hayo ni mambo ya chama na msajili wa vyama, sasa kama barua hiyo ipo wao kinachowafanya waisambaze ni nini? aliyeiandika kwa lengo la kutambulisha maamuzi ya vikao ni Profesa Lipumba ambaye aliituma kwa msajili,  msajili kama kajibu kwa kufuatana na Katiba ya CUF tatizo liko wapi?

“ Ni kweli tumepewa na msajili hiyo barua, hawa wanaoisambaza kwenye mitandao ya kijamii tunajua  wamepewa na vyanzo vyao vya kifisadi huko vinaoweza kuiba nyaraka. 

“Lakini ni kweli hii barua ni ya wazi na si ya siri  hata hivyo hatukuweza kuisambaza kwa sababu haihusiani na wananchi huko nje ni mambo ya chama ya ndani,” alisema Kambaya.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani hapa zinafuatwa sheria na kanuni za CUF, KATIBA ya chama hicho inasemaje ikiwa mwenyekiti kamuita rasmi katibu wake ambaye ni mtendaji mkuu wa chama, na yeye kwa sababu anazozijua hatokei tena bila ya taarifa, japo hata kwa simu? kwanza huu ni ukiukwaji wa kimaadili. pili hapa penda usipende, CUF wanadai waliopo kisiwani ndiyo wa maana na wa BARA, si lolote na si chochote, hali hii wanaifahamu fika na ni moja ambayo ilimuondoa Maalimu kuwa waziri kiongozi kwa kasoro ya ubaguzi tena wa wazi, kati ya wapemba na waunguja, hali hii inaendelea hivyohivyo hata znz kwenyewe CUF wa pemba ni zaidi ya wale wa Unguja, haya ni baadhi ya Masuala yanayoleta matatizo ndani ya CUF. Watu mtapiga kelele sana lakini jaribuni kuangalia kwa sauti na kwa kina.Maalimu na hali ya upemba, uunguja na ubara ndicho chanzo cha kuiua CUF.Chukueni hatua za kuliangaliasuala hili kwa makini na kulitolea majibu baada ya upembuzi yakinifu, kwa maoni yangu haya matatu niliyoyataja ni chanzo kikubwa kwa kukigawa chama hicho. dhambi ya ubaguzi si nzuri sana, na hata ikitokea Maalimu kuwa rais wa znz uenda wenye damu ya kiarabu ndiyo watakaokuwa na nguvu kitu ambacho kitaanzisha mapinduzi mengine kama ya mwaka 1964.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad