Rasmiii..Mayai ya Kizungu na Vifaranga Vyapigwa Marufuku Nchini..!!!


Serikali imesema kuwa hakuna mwekezaji yeyote aliyeruhusiwa kupewa kibali cha kuingiza vifaranga au mayai ya kuku nchini kwa ajili ya biashara.

Katika kusimamia hili, kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67,500 vilivyoingizwa   nchini kinyume na sheria viliteketezwa.

Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvivu, Mhe.William Ole Nasha amesema wapo wawekezaji wachache ambao hupewa vibali maalum vya kuingiza mayai au vifaranga wa kuku wazazi (Parent Stock) pekee na ukaguzi kwa ajili ya kudhibiti uingizaji vifaranga na mayai unaendelea.

Amesema hatua kali zinachukuliwa kwa yeyote anayekamatwa kwa kukiuka utaratibu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad