Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wote wanaojihusisha na uuzaji wa CD za kutembeza mkononi pamoja na wanao-burn miziki ya wasanii kuacha vitendo hivyo kwani vipo kinyume na sheria.
Akiongea katika maandamano ambayo yaliratibiwa na wasanii wa filamu na yeye kualikwa kama mkuu wa Mkoa alikuwa na matamko 7 amboyo yote yamelenga kukemea vitendo hivyo. Aidha ufumbuzi wa tukio hilo ama yoyote anayetaka kuuza filamu za nje inatakiwa wawe na vitambulisho maalumu.
Katika maagizo yote amewataja watu 13 ambao wanahitajika Polisi kwa Siro siku ya ijumaa kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na matumizi ya mitambo ya kudukua filamu. Pamoja na kuzuia filamu za ngono zisiingie mkoa wa Dar es salaam na wasipojipeleka atawafuta mwenyewe.
Amewataka wasanii kufurahia jasho lao kwani wanafanya kazi ya ziada katika kutekeleza kazi zao na kuanzia leo wasanii hao wataanza kunufaika nazo kwani sheria kali na utekelezaji utafuatwa.
Sakata ambalo linaumiza wasanii hao ni uuzaji wa filamu za nje ambazo gharama yake kuanzia 700 kwa bei ya jumla hadi 1000 rejareja.
Sheria ya filamu 1979 inamtaka muuzaji wa filamu za nje na ndani kufuta utaratibu maalum na akitaka kuingiza filamu yoyote lazima ajaze 'form' ya kuomba uingizaji huo