SERIKALI Yakwama Upelelezi kesi ya Wema Sepetu

Leo April 12, Msanii Wema Sepetu alifika katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam kusikiliza kesi ya tuhuma za kutumia na kukutwa na Dawa za kulevya, ambapo UPANDE wa Jamhuri umeshindwa kukamilisha upelelezi dhidi ya kesi inayomkabili msanii huyo.

Upande wa Mashtaka uliowakilishwa na wakili wa Serikali Constantine Kakula, ulidai kuwa kesi hiyo imefika kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika hivyo ipangiwe siku nyingine.

Hakimu  Mkazi Mkuu Thomas Simba, ameuhoji upande wa Jamhuri, kutokana na kuchelewesha upelelezi wa kesi hiyo ambapo kila tarehe inayotajwa Serikali inadai kuwa upelelezi haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa na itatajwa tena tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hamna chochote musitie ila watu wasiokuwa nayo kuvuta bangi mbona wengi tu wanavuta mbona hamuwakamati na kuwa peleka mahakamani jameni kuweni wakweli na sio kudhulumu watu ovyo ovyo WEMA ATABAKI KUWA WEMA NA WEWE BASHITE UTABAKIA HIVO HIVO LETE VYETI HUWEZI KULIKWEPA HILO TUNA TAKA VYETI VYETU

    ReplyDelete
  2. Watakamilishaje mashtaka yasiyo na ushahidi? Itabidi watunge?

    ReplyDelete
  3. Hawana lolote, wanatafuta njia ya kumlinda tu, wanataka ushahidi gani wakati alikutwa na bangi nyumbani kwake na kwenye mkojo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad